loader
Picha

Benki na Airtel kuwezesha kuchukua fedha

BENKI ya Biashara ya Mwalimu imeingia ubia na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, ambapo kuanzia sasa walimu wote ambao ni wateja wa benki hiyo, wataweza kuchukua fedha zao kutoka benki hiyo kwa kutumia huduma ya Airtel Money.

Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money, Isack Nchunda amebainisha hayo jijini Dar es Salaam kuwa lengo la ushirikiano huo ni kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kwa wateja wakiwa popote.

“Walimu ndio idadi kubwa ya wafanyakazi wa serikali hapa Tanzania na pia wako mijini na vijijini hivyo ushirikiano wetu na Benki ya Mwalimu ni hatua moja kubwa zaidi kwenye kutoa suluhisho la huduma za kifedha,” amebainisha.

“Kuanzia sasa walimu wote nchini, hasa wale wa maeneo ya vijijini hawatakuwa tena na sababu ya kutumia siku nzima au kupoteza muda na gharama kusafiri kwenda kufuata mishahara yao benki,” amesema.

Kinachotakiwa kwa mwalimu ni kuunganisha akaunti yake ya Benki ya Mwalimu na Airtel Money, halafu ataweza kuhamishia fedha moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Airtel Money na kuitoa kwa wakala popote alipo.

Alibainisha kuwa muunganiko huo wa huduma za kibenki na huduma za Airtel Money, utawawesha walimu kuweka au kuhamisha fedha kutoka akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti zao Airtel Money, pia kuhamisha fedha kutoka Airtel Money kwenda akaunti ya benki na kutoa fedha kwenye mashine za ATM.

Meneja Biashara wa benki hiyo, Ombeni Kaale alisema “Kwa sasa tunaishi kwenye ulimwengu ambao malipo mbalimbali yanafanyika kila sekunde kwa njia ya simu za mkononi, pia idadi ya wanaolipa kwa mtandao inaongezeka kila siku tena kwa kasi kubwa.

Hivyo ushirikiano wetu na Airtel utatusaidia pia benki yetu kufikia malengo tuliyojiwekea ya kutoa huduma bora na nafuu ambayo inaendana na mahitaji ya wateja wetu kila siku”.

WAKULIMA 34 mkoani Njombe wamezalisha miche 4,500 ya miparachichi kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi