loader
Picha

Wahamiaji haramu 6 wakamatwa Mwanza

IDARA ya Uhamiaji mkoani Mwanza imewakamata watu sita wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu, katika operesheni yake iliyoendeshwa jijini humo kati ya Machi 17 hadi 23, mwaka huu.

Ofisa Uhamiaji Mkoa, Kamishina Msaidizi wa Uhamiaji, Bahati Mwaifuge alisema hayo jana hapa alipozungumza na waandishi wa habari juu ya hatua wanazochukua kudhibiti wahamiaji haramu.

Mwaifuge alisema kati ya wahamiaji hao waliokamatwa, watatu ni kutoka Burundi, wawili kutoka Tanzania na mhamiaji mmoja mmoja kutoka nchi za Kenya na Rwanda.

“Kwa wahamiaji haramu wa Tanzania, uraia wao bado una utata na mhamiaji haramu wa Burundi amesharudishwa kwao,” alisema.

Pia alitoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizogaa mitandaoni za kuwepo kwa watu tisa wanaodaiwa ni wafanyabiashara wa jijini Mwanza waliorudishwa nchini na Serikali ya Uganda.

Kuhusu madai ya wafanyabiashara tisa kurudishwa nchini kupitia bandari ya Mwanza na Serikali ya Uganda kwa kuhofia ugonjwa wa corona kutokana na taarifa zilizozagaa na kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii alisema taarifa hizo si za kweli bali zina lengo la kuipotosha jamii.

Mwaifuge alisema watu hao tisa ni wafanyakazi wa meli ya mizigo ya Mv Upendo waliondoka nchini Februari 16, mwaka huu kabla nchi haijapata maambukizi ya corona wakisafirisha mizigo Jinja, Uganda.

Alisema waliposhusha mizigo Uganda, walienda Kisumu, Kenya na walirudi wiki hii kutoka Uganda.

“Walipofika bandarini wakielekea Jinja nchini Uganda, walizuiwa na polisi kwa ajili ya kupima afya zao na walipima na kubainika hawana maambukizi ya ugonjwa wa corona,” alisema.

Alisema nahodha wa meli hiyo, Juma Mchalaganya na Mkurugenzi wa meli hiyo, Timothy Kilumile na walimthibitishia kuwa wale hawakuwa wafanyabiashara bali walikuwa ni wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye meli hiyo ya mizigo na wako salama na wanaendelea na shughuli zao kwa mujibu wa sheria.

“Nitumie fursa hii kuwaomba waandishi wa habari kabla hawajatoa taarifa yoyote kwenda kwa umma, hasa kwa wakati huu waifanyie utafiti wa kina na kuuliza mamlaka zinazohusika,” aliongeza.

Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa meli ya Mv- Upendo, Timothy Kilumile alisema binafsi ameshitushwa na taarifa hizo za wafanyabiashara waliorudishwa Mwanza. Alisema ukweli ni kuwa hakuna wafanyabiashara waliorudishwa na Serikali ya Uganda jijini Mwanza kwa kuhofia Corona.

“Wanaodaiwa ni wafanyabiashara ni wafanyakazi tisa wa meli yangu na hawajawahi kurudishwa Mwanza, bali waliondoka Mwanza Februari 16 kusafirisha mizigo kwenda Jinja, Uganda,” alisema.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi