loader
Picha

Eze Nice kuachia nyimbo mbili

MSANII wa muziki wa bongo fl eva, Ezra Msiliova ‘Eze Nice’ amewaomba wadau wa muziki huo kupokea nyimbo zake mbili anazotarajia kutoa hivi karibuni.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mkoa wa Iringa, Eze Nice alisema kuwa nyimbo hizo ni zawadi kwa Rais Dk John Magufuli na mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas’ na ameziita Magufuli na Asas.

Alisema wimbo wa kwanza ni Magufuli unaeolezea kazi zilizofanywa na Rais kwa kipindi hiki na wimbo wa pili ni zawadi kwa Salim Abri ambaye amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa Mkoa wa Iringa, hivyo kuwaenzi ametunga nyimbo hizo na zinatarajia kuwa kali kwani ziko katika mahadhi ya rhumba na ni nzuri kucheza na kusikiliza ujumbe wake.

“Hawa watu wamefanya makubwa Tanzania na mkoa wetu kwa kweli hiyo ni zawadi nawapa kila mmoja kwa kuwa na wimbo wake na kusema malengo yake ni kuwa msanii mkubwa katika sanaa ya muziki na nia ninayo kufikisha muziki mbali zaidi kuliko ilivyo sasa,” alisema.

Pia alishukuru vyombo vya habari kwa kuzipiga na kuandika habari zake na kutoa wito kwa wasanii wengine kutokata tamaa kwa kuwa sanaa inahitaji nidhamu, heshima na uvumilivu ili kufikia malengo.

WAKATI Yanga ikiendelea na mazungumzo ya kumbakisha nahodha wao, Papy ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi