loader
Picha

Maji Ziwa Tanganyika yakimbiza familia za watu 90

FAMILIA zinazokadiriwa kuwa na watu 90 zimekimbia nyumba zao baada ya Ziwa Tanganyika kujaa maji na kusababisha mafuriko. Nyumba 18 zilizojengwa maeneo ambayo awali Ziwa Tanganyika lilikuwa linafika kijiji cha Kirando wilayani Nkasi zimejaa maji.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Diwani wa Kata ya Kirando, Kakuli Seba alisema maji ya Ziwa Tanganyika yamefika maeneo lililokuwa miaka 30 iliyopita na kusababisha mafuriko.

Aliongeza kuwa pia majengo ya kituo cha mafuta, hoteli ya Nkondwe Beach, mwalo wa samaki na gati yamefurika maji. “Hoteli ya Nkondwe Beach imefurika maji na imelazimika kufungwa. Yaani ukiacha milango wazi samaki wanaingia chumbani ...unaweza kuwavua. Pia biashara ya samaki imekuwa ngumu baada ya mwalo wa samaki kufurika maji,” anaeleza.

Wakizungumza na gazeti hili, wavuvi wa samaki wamesema changamoto kubwa ni mafuriko hayo ambayo yamesababisha biashara ya samaki kuwa ngumu.

“Hatuwezi kufika mwaloni. Maji kutoka Ziwa Tanganyika yamefurika hapo, hakuna tena biashara ya samaki,” alisema mvuvi wa samaki, Johnson Kapela.

NTAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoa ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Nkasi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi