loader
Picha

Wawili wauawa singida vifo vya kutatanisha

WATU wawili wameuawa mkoani Singida katika matukio tofauti ya kutatanisha Machi 18 na 23 mwaka huu. Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike (pichani) alisema kuwa katika tukio la Machi 18, mwaka huu, mwili wa Lissu Abdallah, mkazi wa kijiji cha Mnolo wilayani Mkalama mkoani hapa uliokotwa na raia wema ukiwa umetelekezwa pembeni mwa Mto Ndurumo katika kijiji cha Msingi wilayani humo.

Alisema kuwa baada ya mwili huo kukosa mtu wa kuutambua, ulizikwa lakini ukafukuliwa baada ya ndugu zake kujitokeza siku 10 baadaye. Kamanda Njewike alisema kuwa baada ya mwili wa marehemu Lissu kuchunguzwa na daktari, alibaini kifo chake kilisababishwa na shingo kuvunjwa na kwamba mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Ilielezwa Lissu aliondoka kijijini kwao Machi 17 akiwa na gari ndogo aina ya Opah lenye namba za usajili T462 DCH lakini hakurejea tena hadi mwili wake ulipookotwa kijiji cha Msingi wakati gari lake likiwa limetelekezwa kijiji cha Misigiri barabara kuu ya Singida – Mwanza, zaidi ya kilometa 30 kutoka eneo mwili wake ulipookotwa.

Katika tukio la pili Machi 23 mwaka huu, mwili wa Fadhila Ibrahim (19) ambaye ni mke wa dereva wa bodaboda, Abubakar Hamis (25) mkazi wa eneo la Mnung’una Manispaa ya Singida uliokotwa ukiwa umetelekezwa kwenye korongo lenye maji eneo la Kona ya Mohammed mjini hapa, umbali wa kilometa tano hivi kutoka makazi ya wanandoa hao.

Alieleza baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi, ulikutwa hauna jeraha lolote isipokuwa mapovu mdomoni hali iliyotia shaka; hivyo kumkamata mume wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

NTAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoa ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Singida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi