loader
Picha

Watendaji tekelezeni agizo Majaliwa kukabili Corona

JUZI Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kamati za maafa katika ngazi za mikoa na wilaya zote nchini kuungana na waratibu wa wa serikali kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya COVID-19 wanaopatikana katika maeneo yao.

Kati ya maagizo yake, ni kuangaliwa upya mkakati wa kukabiliana na ugonjwa wa Corona unaolazimisha kuwekwa karantini kwa wageni wanaoingia nchini ambapo kwa sasa hupelekwa katika hoteli za bei ya juu.

Katika hili, Waziri Mkuu ameagiza wapelekwe kwenye gharama nafuu hasa wanazozichagua wao. Binafsi ninaungana na Waziri Mkuu katika jitihada zake za kuhakikisha ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kubwa duniani hauleti kero zaidi kwa Watanzania na wageni, hasa wanapokuwa wametengwa kusubiri majibu ya vipimo vyao.

Huku tayari kukiwa na wagonjwa 13 hadi sasa nchini na kukiwa hakuna kifo hata kimoja ambapo kwa sasa Marekani ndio ina idadi kubwa ya wagonjwa na hadi jana, ilikuwa na wagonjwa wapya zaidi ya 130, ikiwa na kesi 104,256 na vifo 1,704 wakati waliopona ni 2,525.

Hivyo ni wazi kuwa watendaji wa serikali katika ngazi mbalimbali nchini wanapaswa kuongeza umakini zaidi katika kuzuia maambukizi mapya ya ugonjwa huo. Kwa kuwa serikali inao wataalamu kadhaa wa afya katika kila kona ya nchi ni muda mwafaka kwa watendaji hao kushirikiana na wataalamu hao kuielimisha jamii njia bora za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Wanapaswa kuhakikisha wananchi wanatumia vitakasa mikono pamoja na kunawa kwa kutumia sabuni na maji yanayotiririka, lakini sio tu kuhakikisha huduma hizo zinakuwepo ila zinatumiwa kikamilifu na watu.

Ni wazi kuwa watendaji wana nguvu za kimamlaka, hivyo wanaweza kulazimisha wananchi wanazigatia taratibu za kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa huo.

Watendaji wanapaswa kuhakikisha kuwa shughuli za kimaendeleo zinaendelea kama kawaida kwa kufanya kazi kwa bidii huku wakiendelea kujilinda.

Haimaanishi kuwa kwa kuwa wameachwa kuendelea kuwepo mitaani tofauti na ilivyo kwa nchi za Ulaya na Marekani ambapo wananchi wanakaa ndani muda wote, ndio iwe sababu ya kusababisha mikusanyiko isiyokuwa ya lazima kama vile kwenda baa na kwengineko.

Haya yote yanaweza kufanyika iwapo kama watendaji hao kuanzia ngazi za vijiji, kata, wilaya na mikoa kuongeza umakini katika kuelimisha jamii.

MAPEMA mwezi huu vyama mbalimbali vya siasa nchini, vimepuliza kipenga ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi