loader
Picha

Wachezaji Simba kukutana kupanga mikakati

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wanatarajiwa kukutana wiki ijayo kuweka mikakati ya namna gani ya kusonga mbele.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema wanatarajia kukutana kesho kutwa na wachezaji wote hivyo, wataamua wafanye nini kujiimarisha katika michezo ijayo ya ligi.

Alisema watakutana na timu zote za wanaume, wanawake na vijana ambao hivi karibuni baada ya serikali kutangaza kusitisha mikusanyiko na michezo yote kwa siku , uongozi wa klabu hiyo uliwaruhusu wachezaji wote wakapumzike kwa muda.

“Tutakuwa na kikao Jumanne na timu zote za Simba kuangalia ni kwa namna gana tunaweza kusonga mbele na kujipanga kwa programu na kujiweka tayari kwa michezo ijayo,” amesema.

Mazingisa alisema wana kazi kubwa kuhakikisha wanajiandaa kuendeleza ushindi katika michezo ijayo ya ligi na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), hivyo ni lazima wawe na mikakati ya kuifanya timu kuwa tayari.

Wekundu hao wamekuwa katika kiwango bora tangu kuanza kwa ligi wakiongoza kwa pointi 71 katika michezo 28 waliyocheza wakiwaacha wapinzani wao mbali.

Azam FC inashika nafasi ya pili kwa pointi 54 katika michezo sawa na Simba, na Yanga ipo nafasi ya tatu kwa pointi 51 katika michezo 27.

Pointi nyingi ilizonazo Simba inapewa uwezekano wa kulitetea taji hilo kwa mara nyingine na kuwakilisha nchi mwakani kimataifa.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi