loader
Picha

Tshishimbi, Morrison hakuna kulala

WAKATI baadhi ya wachezaji wazawa wa Yanga wakila bata kufuatia mapumziko ya siku 30 za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona wachezaji wa kimataifa wa timu hiyo wameendelea kujifua kwa mazoezi kulinda viwango vyao.

Wachezaji Papy Tshishimbi na Bernard Morrison wameonesha ni namna gani wanathamini kazi yao kwa kufanya mazoezi kusaidia kubaki katika kiwango bora pindi ligi itakapoendelea.

Tshishimbi ameonekana akijifua kwenye gym moja nchini, kitu ambacho kimeonesha amepania kulinda kiwango chake na kuisaidia timu yake kufanya vizuri kwenye mechi za ligi.

“Mpira ni kazi yangu, hivyo ni lazima nifanye mazoezi kulinda kiwango changu na kuisaidia timu yangu kufikia malengo na siri kubwa ya kuendelea kuwa bora ni mazoezi tu hakuna lingine,” alisema Tshishimbi.

Mchezaji huyo aliyejiunga na Yanga mwaka juzi akitokea Mbabane, amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho huku mwenyewe akisema siri ya ubora huo ni mazoezi.

Morrison alionekana anajifua sehemu ya wazi kwa kuruka.

Ikumbukwe mchezaji huyo aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo hivi karibuni, ameongeza mkataba wa miaka miwili ikiwa ni muda mfupi baada ya kuibuka shujaa kwenye mchezo wa watani zao Simba baada ya kufunga bao pekee.

Ligi zote zimesimama kwa siku 30 ikiwa ni agizo la serikali lililotolewa hivi karibuni kuepuka kuenea kwa virusi vya corona katika mikusanyiko ya watu.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi