loader
Picha

Wachezaji Azam kujieleza

WACHEZAJI wa Azam FC watakaoshindwa kuzingatia programu walizopewa kipindi hiki cha mapumziko ya siku 30 wanaweza kuchukuliwa hatua kali.

Kabla ya kupewa mapumziko hayo ya serikali kwa ajili ya kupunguza kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona, Kocha wa Azam, Aristica Cioaba aliwapa wachezaji wote programu ya kufanya itakayosaidia kulinda viwango vyao.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Azam FC, Zakaria Zakazi amesema kutokana na maelekezo yaliyotolewa anaamini wachezaji hao watazingatia kwa manufaa yao na timu.

“Kila mchezaji alipewa programu yake akafanye nyumbani na wakaelezwa mapema kama kuna ambaye anajiona hawezi basi abaki asiondoke lakini wengi waliahidi kufanya,”amesema.

Zakazi amesema kwa ajili ya kufuatilia kweli wanafanya walichoelekezwa walielezwa kuandika ripoti zao za kila wiki na kutuma kwa kocha wao.

Pia amesema ambaye atashindwa kufanya kile alichoelekezwa atatakiwa kujieleza ili aweze kueleweka.

Amesema wanataka wakirudi wawe katika kiwango bora kitakachowezesha kupambana katika mechi zilizobakia na kufanya vizuri.

Wanalambalamba hao wanatarajiwa kurudi kambini baada ya kumaliza siku 30 zilizotangazwa na serikali kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu itakayochezwa baadaye bila mashabiki kutokana na hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa corona.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi