loader
Picha

Mwanamuziki Norway kukipaisha Kiswahili

MWANAMUZIKI mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayefanya shughuli zake za muziki nchini Norway, Andrew Ripper ameonesha nia ya kufanya kazi na wasanii wa hapa nchini kwa lugha ya Kiswahili.

Ripper ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo kama vile Dance Together na Jack and Rose ambazo zimeshika chati katika kumi bora ya Mtv kwa ukanda wa Afrika na Mtv duniani.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao akiwa Norway, alisema amekuwa akifuatilia muziki wa hapa nchini hasa wasanii kama akina, Ali Kiba, Mimi Mars, Raymond Mwakyusa (Ray- Vanny), Rajabu Kahali (Harmonize), Elias Barnaba (Barnaba Classic), Vanessa Mdee na wengine wengi.

“Natambua nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki na ndio maana nimekuwa nikitumia lugha hii na nawaomba wasanii wa Tanzania kuwa tayari kufanya kazi za muziki na mimi,” alisema.

Alisema kufanya kazi na wasanii wa hapa nchini itasaidia kuwatangaza nchini Norway kwani kuna fursa nyingi katika muziki hasa matamasha.

Aliyataja matamasha makubwa ya muziki ambayo hata wasanii wa hapa nchini anaweza kuwatafutia nafasi ni tamasha la muziki la Oslo, Canal Street, Kilden Street House, tamasha ambalo ni kati ya matamasha makubwa nchini Norway ambayo wasanii wengi wakubwa kama vile Wyclef Jean, Salif Keita, Timbuktu, Madcom, Philip Emilio wamewahi kushiriki.

Pia alisema ameamua kuimba kwa lugha ya Kiswahili baadhi ya nyimbo zake na na ataendelea kutangaza Kiswahili na kusema virusi vya corona vikiishe atakuja Tanzania kwa kazi zaidi.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi