loader
Picha

Corona yaharibu mipango ya bondia

BONDIA Bruno Tarimo ‘Vifua viwili’ amesema ugonjwa wa virusi vya corona umesababisha pambano lake la mkanda wa mabara lililopangwa kufanyika nchini Australia kuahirishwa.

Tarimo anayeishi Australia kwa sasa, amesema michezo imesimamishwa kwa miezi sita ikiwa ni pamoja na mazoezi na ofisi mbalimbali zimefungwa.

Akizungumza na gazeti hili jana amesema alikuwa anatamani kuendelea kushiriki mapambano makubwa na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania ila ugonjwa huo umekuwa ni kikwazo.

“Nilikuwa najiandaa vyema kwa mazoezi makali kwa ajili ya pambano hilo kubwa la mabara kulivyotokea virusi vya corona kila kitu kikaharibika, nilikuwa natamani kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania,”alisema.

Alisema hawana budi kujihadhari kwa ugonjwa huo na hapaswi kudharau maamuzi yaliyofanyika kwa sababu hata mataifa mengine watu wamekuwa hawatoki ndani.

Bondia huyo alisema yeye bado ana ndoto za kufikia kiwango cha juu kama walivyofika Manny Pacquiao wa Ufilipino na Myweather wa Marekani.

Alisema kusimamishwa kwa mazoezi hakutamfanya arudi nyuma bali atapambana awezavyo kuendelea na mazoezi baadaye na kufanya kile anachokitaka.

Tangu afike Australia mwaka 2018 ameshiriki mapambano ya ushindani sita na kati ya hayo, ameshinda matano.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi