loader
Picha

Corona pigo soka England

MAAMUZI magumu yaliyochukuliwa ili kukabiliana na virusi vya corona katika soka la England, ni pigo kwa Ligi Kuu, EFL, na Chama cha Wachezaji wa Soka la Kulipwa.

Pigo hilo ni kutokana na mechi zote kusimamishwa hadi Aprili 30 na kwamba uwezekano wa ligi hiyo kuendelea kunategemea hali halisi ya mambo yatakavyokuwa kwa kuwa ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kwa nchi hiyo ambapo tayari Prince Charles na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Boris Johnson wameathirika na ugonjwa huo.

Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa walisema katika taarifa yao ya pamoja kuwa wanafikiri kila mtu anaweza kuathirika na virusi vya corona.

“Tulikubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili tuweze kufikia muafaka,“ taarifa ya pamoja ilisema. Mkutano mwingine umepangwa kufanyika wiki ijayo ili kupata suluhisho la pamoja la kupambana na hali ngumu inayozikabili ligi hizo, klabu, wachezaji, wafanyakazi na mashabiki.

Klabu za Ligi Kuu ziko tayari kukutana tena Aprili 3, na huenda mapumziko yake yakaendelea zaidi ya Aprili 30. Kuongezeka kwa idadi ya siku za kusubiri kunahatarisha tarehe ya kumalizika kwa ligi hiyo pendwa duniani zaidi ya kipindi chake rasmi cha msimu wa Ligi Daraja la Kwanza, ambao ulitakiwa kuwa Mei 17.

Wachezaji katika baadhi ya klabu za Ulaya, ikiwemo Bayern Munich na Borussia Dortmund wote kwa pamoja wamekubali kukatwa kwa muda mapato yao.

Wakati hatma ya Ligi Kuu na ile ya Daraja la Kawanza haijulikani, Chama cha Soka tayari kimefutilia mbali mechi zote zisizo za ligi. Zaidi ya klabu 30 ziko tayari kupinga uamuzi huo, wenye maana kuwa hakutakuwa na timu itakayopanda daraja au kuteremshwa, hatua ambayo bado haijaelezwa na FA.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi