loader
Picha

Mbosso awajengea nyumba wazazi wake

MSANII wa muziki Bongo fleva, Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ amekamilisha kuwajengea wazazi wake nyumba ya kuishi.

Kwa mujibu wa video aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram jana, Mbosso yupo na baba yake mzazi, Kiyungi katika nyumba hiyo mpya ambayo imekamilika kila kitu na kujengewa ukuta.

“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kunipa nguvu ya kutimiza ndoto hii kwa ajili ya wazazi wangu,” aliandika Mbosso na kuendelea.

“Leo hii wazazi wangu wanaanza kukaa kwenye nyumba ambayo mtoto wao nimewajengea kwa jasho langu, asante Mola wangu,” aliongeza Katika video ya hiyo Mbosso yupo na baba yake mzazi, Kilungi ambapo baba yake akimkumbusha kununua kiwanja kingine na Mbosso akamjibu asiwe na haraka. Februari 20 mwaka huu, Mboso alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram :

“Nimebakisha sehemu ndogo wazazi wangu, ila nikijaliwa nitafanikisha kwa uwezo wa Mungu, ni zawadi gani nzuri ambayo unatamani siku moja kuwapatia wazazi wako?”

Miongoni mwa watu walifurahishwa na hatua ya Mbosso ni Diamond Platnumz na aliyesema:

“Hii ni Baraka kubwa, Mwenyezi Mungu atusimamie, na azidi kutubariki katika kazi zetu na kila anayetukusudia ubaya amlipe anachostahili”.

Januari, 29, 2018 Mbosso alitambulishwa kuwa msanii wa WCB baada ya kusaini mkataba baada ya kundi lao la Yamoto bendi kufa.

Hadi sasa Mbosso ametoa nyimbo kama vile Watakubali, Nimekuzoea, Alele, Shida, Picha yake, Hodari, Nipepe, Hodari, Tamu.

Wimbo mwingine aliotoa na kundi la Wasafi ni Zilipendwa na Jibebe.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi