loader
Picha

Khadija Kopa autamani ubunge

MWIMBAJI wa muziki wa Taarab, Khadija Kopa amesema anatarajia kuwania ubunge kupitia Viti Maalumu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Khadija alisema amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kwa miaka 10 hivyo siasa anaifahamu.

“Natamani nigombee ubunge kupitia viti maalumu, lakini bado sijajishauri vizuri,” alisema kwenye kipindi cha Salama kinachorushwa na EATV.

“Mimi huku bara nimekuwa mwenyeji, na nimekaa miaka mingi, hivyo kama nitagombea nitagombea kupitia huku bara,” alisema.

Malkia huyo wa mipasho anatamba na wimbo wa Wigi Linawasha ambao aliutoa mwanzoni mwa mwaka jana.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi