loader
Picha

Mwasiti: Wimbo na Chid Benz ulinipa mafanikio

MSANII wa muziki wa Bongo fl eva, Mwasiti Almasi amesema wimbo wake wa ‘Hao’ aliomshirikisha Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ ulimpa mafanikio makubwa kwenye muziki kwani ulimwezesha kufanya tamasha kubwa Afrika mbele ya Marais wengi barani Afrika.

Akizungumza juzi katika kipindi cha Dadaz kinachorushwa na EATV, Mwasiti amesema wakati akifikiria kutoa wimbo huo na Chid Benzi uongozi wake wa kipindi hicho haukuwa tayari.

“Nakumbuka wakati napeleka wimbo wangu na Chid Benzi kwa bosi wangu, aliniambia ule siyo saizi yangu, ila alipo ruhusu upigwe, ndani ya wiki moja tu ukanifanya kuwa msanii mkubwa Afrika kwa sababu nilipata nafasi ya kufanya tamasha kubwa Ethiopia mbele ya Marais wote Afrika,” alisema Mwasiti.

“Baada ya hayo mafanikio nikaamua kuwa Mwasiti wa sasa japo kuna wasanii wananiona mimi mshamba,” aliongeza Mwasiti.

Mwasiti ambaye pia ni mwandishi wa nyimbo za Afropop, Zouk na Bongo Fleva mwaka 2009 alitwaa tuzo ya wimbo bora wa zouk kupitia wimbo wa Nalivua Pendo ambao ulishika namba moja kwenye chati za wimbo bora kwa wiki nane mfululizo.

KLABU ya Tottenham imepata mkopo wa Pauni milioni 175 sawa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi