loader
Picha

Wakulima wazalisha miche 4,500 ya maparachichi

WAKULIMA 34 mkoani Njombe wamezalisha miche 4,500 ya miparachichi kwa teknolojia walizofundishwa na Taasisi ya Utafi ti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Uyole Mbeya.

Uzalishaji wa miche hiyo 4,500 utamwezesha kila mkulima kupanda miche 200 kwenye shamba la eka mbili kuongeza kipato cha mtu mmoja na taifa.

Miche hiyo iligawiwa kijiji cha Igongolo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Uyole, Dk. Tulole Bucheyeki.

Akizungumza na HabariLeo, Dk Bucheyeki alisema miche hiyo 4,500 itapandwa kwenye eneo la eka 70 hivyo kwa miaka minne ijayo wakulima hao watatarajia kuvuna tani tisa za matunda ambapo kwa kilo maparachichi hayo yakiuzwa kwa kilo sh. 1500 zitapatikana Sh milioni 13.5.

“Lakini miaka saba ijayo miche hiyo inaweza kutoa mavuno ya tani 10,335 na yakiuzwa sh. 1,500 kwa kilo zitapatikana zaidi ya Sh bilioni moja… katika mapato hayo halmashauri na serikali kwa ujumla itaweza kupata kodi ya Sh milioni 46 ndio maana nasema ni miti fedha,” amesema Mkurugenzi huyo.

Kuhusu soko, Dk Bucheyeki alisema soko la parachichi ni kubwa kwani hivi sasa Tanzania kuna watu milioni 50, endapo kila mwananchi atakula parachichi 100 kwa mwaka mzima maana yake maparachichi yote yatakayozalishwa yataisha.

Pia alihamasisha watanzania kuuza maparachichi ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vya kuchakata. Mratibu wa utafiti kituoni hapo, Dk Ndabhemeye Mlengera alisema kilimo cha parachichi ni tofauti na mazao kama mahindi na maharage yanayolimwa kwa msimu.

Alisema kwa parachichi hata kama mkulima ana mimea michache na uhakika wa kuvuna kila mwaka miaka inavyozidi ndio mapato ya matunda yanaongezeka.

Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Editha Mligo alisema ili kufanikiwa lazima kuwe na ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi.

Kwani halmashauri hiyo inashirikiana na wadau zaidi ya 40 katika kufanikisha maendeleo ya kilimo kikiwemo kituo hicho cha Uyole.

Mtafiti wa matunda na mbogamboga kituoni hapo, Daud Mbongo amesema wamewapelekea wakulima hao aina sita za miche ya miparachichi ambayo ni Ikulu, Hass, Fuerte, Simons, Uyole Line na Wese na kati ya hizo walichagua aina aina tatu.

Mkulima wa maparachichi, Fanueli Salingo amesema tangu walipoanza kupanda miparachichi kipato chao kimeongezeka na kuweza kusomesha watoto wao, ndio maana wameona kuna haja ya kuendelea kulima zao hilo.

Kaimu Mratibu wa Uhaulishaji wa Tekinolojia na Mahusiano, Kissa Mwaisoba alitoa wito kwa mashirika na taasisi zisizo za kiserikali kununua miche bora na kupata elimu juu ya kilimo cha miparachichi katika kituo hicho cha utafiti Uyole.

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Shirika ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi