loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Visima 20 kuchimbwa shuleni Zanzibar

ASASI ya Time To Help kwa kushirikiana na Shule ya Feza na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, wamezindua mradi wa visima virefu vya maji katika shule za msingi na sekondari visiwani Zanzibar.

Mradi huo ambao utakaotekelezwa mwaka huu, utahusisha uchimbaji wa visima 20 shuleni na utagharimu Sh milioni 150.

Uzinduzi wa mradi huo ulifanya na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Simai Mohamed Said kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia viongozi wa wizara hiyo, viongozi wa Wizara ya Utumishi wa Umma Zanzibar, Mwenyekiti wa taasisi ya SABIL ambao ndio wamiliki wa Shule za Feza Zanzibar, Mwalimu Mkuu wa shule ya Feza Zanzibar, Ali Nungu na Mwenyekiti wa Asasi ya Time To Help, Ramadhani Praph.

Katibu Mkuu wa Asasi ya Time To Help, Ramadhani Praph alisema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita taasisi hizi mbili (Time To Help na Shule Feza), zimeshachimba visima 30 Zanzibar.

Mwaka huu wameweka malengo ya kuchimba visima 20 shuleni. Alisema mpaka sasa maeneo 14 yameshatengwa kwa ajili ya uchimbaji wa visima hivyo 20 na maeneo sita bado.

Kwamba katika malengo yao ya visima 20, visima vinne tayari vimeshachimbwa na kuzinduliwa katika shule za Sekondari Muanda na Wete, Pujıni na Mizingani Msingi na Sekondari.

Visima vitatu ambavyo uchimbaji wake unaendelea ni vya Shule za Sekondari ya Mgambo na Shule za msingi Kijumbani na Skuli ya Msingi Sebleni.

Alisema lengo la kujenga visima shuleni ni kusaidia harakati za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuboresha elimu kwa kupeleka majisafi na salama shuleni, ambako kutapunguza usumbufu na kupoteza muda kwa wanafunzi katika kutafuta maji.

Alisema muda huo utatumika katika kujifunza zaidi, hivyo kuongeza ufaulu wa masomo.

Aliongeza kuwa wanafunzi wakiwa na majisafi na salama shuleni, itasaidia kujikinga na maradhi mbalimbali kama virusi vya corona.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Simai ameshukuru Time To Help na shule za Feza kwa msaada huo wa upelekaji wa vyanzo vya maji shuleni.

Simai amesema vyanzo hivyo vya maji vitasaidia kutatua kero ya upatikanaji wa maji shuleni na wananchi wanaozizunguka shule hizo, hivyo kuleta tija katika kuboresha elimu na afya ya wanafunzi na wananchi.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Abdullah Abdullah, aliishuku Time To Help na Shule za Feza.

Ameomba kudumishwa kwa ushirikiano baina ya taasisi hizo na Wizara ya Elimu katika nyanja nyingine, ambazo asasi ya Time To Help inajishugulisha.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi