loader
Dk Mpango: Washiriki wa maendeleo hutumiza ahadi

Dk Mpango: Washiriki wa maendeleo hutumiza ahadi

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philipo Mpango (pichani) amesema sio sahihi hata kidogo kusema kwamba kuna nyakati zingine washiriki wa maendeleo wamekuwa hawatimizi ahadi zao kabisa.

Dk Mpango aliyasema hayo wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema). Silinde alisema: “Nchi wahisani na washirika wa maendeleo wamekuwa wakishindwa kuleta misaada na ahadi zao kwenye utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo kwa wakati na nyakati nyingine kushindwa kuleta kabisa katika kipindi cha miaka mitatu ya fedha mfululizo iliyopita ya 2016/2017, 2017/2018 na 2018/2019.”

Hivyo Siline alitaka kupata maelezo ya serikali ya ni kitu gani kinasababisha hali hiyo. Akijibu swali hilo, Mipango alisema Serikali imekuwa ikishirikiana na nchi wahisani pamoja na washirika wa maendeleo katika kutekeleza Bajeti yake kwa kupokea fedha za Bajeti ya Maendeleo kupitia Misaada na Mikopo nafuu kwa mujibu wa makubaliano ya kimkataba.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia 2016/17 hadi 2018/19 Washirika wa Maendeleo wamekuwa wakitimiza ahadi zao kwa wastani wa zaidi ya asilimia 77.

Akifafanua zaidi, Dk Mipango alisema kiasi kilichopokelewa kutoka kwa washirika wa maendeleo kwa mwaka 2016/17 na Sh bilioni 2,474 sawa na asilimia 69 ya lengo la kipindi hicho la kupokea Sh bilioni 3,601.

Alisema kwa mwaka 2017/18 kiasi kilichopokelewa kilikuwa ni Sh bilioni 3,351 sawa na asilimia 84 ya lengo la kipindi hicho la kupokea Sh bilioni 3,971 na mwaka 2018/19 kiasi kilichopokelewa ni Sh bilioni 2,082 sawa na asilimia 78 ya lengo la kipindi hicho la kupokea Sh bilioni 2,676.

“ Aidha, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2019 hadi Februari, 2020 fedha za misaada na mikopo nafuu zilizopokelewa kutoka kwa Washirika wa Maendeleo zimefikia jumla ya shilingi bilioni 1,631.19 sawa na asilimia 90 ya lengo la kipindi hicho.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f22203bc9ac6b57fd5ba7fe42a1d840c.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi