loader
Picha

Mamia, madaktari Z'bar wawekwa karantini

WATU 324 wamewekwa katika sehemu maalumu ya uangalizi, wakiwemo wauguzi na madaktari 27, kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ugonjwa huo na hatua zilizofikiwa hadi sasa.

Amesema wahudumu wa afya na madaktari 27 wanaochunguzwa afya zao ni wale ambao kwa njia moja au nyingine waliwahudumia watu walioambukizwa na maradhi hayo.

‘’Wapo watu 324 tunawachunguza afya zao na wapo chini ya uangalizi maalumu, lakini pia wapo wauguzi na madaktari 27 ambao hao walitoa huduma kwa watu walioambukizwa virusi vya corona,” amesema.

Alisema hadi juzi kulikuwa na wagonjwa watano wa corona na wamelazwa katika kambi maalumu iliyopo Kidimni na hali zao zinaendelea vizuri.

Aidha, Waziri huyo alisema serikali ya Zanzibar imechukua uamuzi wa kufunga nyumba za starehe,vikiwemo vilabu vya pombe ili kuepusha kuenea kwa maambukuzi ya virusi vya corona.

Alisema kufungwa kwa sehemu hizo, lengo lake kubwa ni kupunguza mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, ambayo ni moja ya chanzo cha kuenea kwa ugonjwa huo.

“Tunawaomba wananchi kwa ujumla wawe wasikivu huku wakisilikiza maagizo ya viongozi wakuu katika kupambana na virusi vya corona, tupunguze mikusanyiko isiyokuwa na sababu,” alisema.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar, Dk Jamala Adam Kassim, aliwataka wananchi kuchukuwa tahadhari zote wakati wanapoingia katika jengo la hospitali hiyo kwa ajili ya kupata huduma za afya pamoja na kuangalia wagonjwa.

Alisema baadhi ya watu wanakiuka maagizo ya afya yanayotolewa na uongozi wa hospitali hiyo, ikiwamo kuwatembelea wagonjwa wakiwa zaidi ya watu watatu.

NTAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi