loader
Picha

Mkurugenzi- Watumishi TFS hamtabaki salama

MKURUGENZI wa Wakala wa Misitu Tanzania, TFS, Santos Salayo ameonya watumishi wanaosaidia wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa ushuru wa serikali kwamba hawatabaki salama.

Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi huyo, kwenye kikao kazi cha watumishi wa TFS mjini Rufiji kwa ajili ya kupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu yao.

Salayo amesema taasisi hiyo haitavumilia watu wanaoishi kiujanja na kwamba kila atakayebainika hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.

Aliwataka watumishi kutekeleza wajibu na majukumu yao kama ipasavyo ili kuondoa malalamiko na tuhuma ambazo zimekuwa zikiwachafua wao,TFS na serikali kwa ujumla.

Meneja wa TFS Wilaya ya Rufiji, Safihu Hamza amesema wao wapo tayari kutekeleza maagizo ya serikali na kusimamia mapato kutokana na shughuli za misitu.

Hamza pia alielezea mpango mkakati wa kudhibiti mazingira kwa kupanda miti maeneo mbalimbali ya umma na kuelezea mafanikio kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo alisema zaidi ya miti elfu 20 ilipandwa.

Aidha alisema kwa mwaka huu kumekuwa na changamoyo katika upandaji miti kutokana na kuzuiamkwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Alisema kazi hiyo itaanza mara baada ya zuio la serikali kuondolewa na shule kufunguliwa .

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Shirika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Rufiji

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi