loader
Picha

Tuwe makini kudhibiti watoto kujikinga na Covid-19

MAPAMBANO ya ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) yanaendelea duniani kote kila nchi ikichukua tahadhari kuwalinda raia wake kwa namna inavyofaa kwa kuzingatia mazingira yake.

Pamoja na ukweli huo kutokana na idadi kubwa ya watu walifariki kuwa wazee, ipo sababu ya makusudi inayostahili kuchukuliwa kuwalinda wazee dhidi ya ugonjwa huo. Katika kundi ambalo halina wasiwasi ni kundi la watoto ambao kiukweli hawajui nini kinaendelea duniani hapa pamoja na kuona katika televisheni na kusoma katika magazeti.

Licha ya watoto kuwa na mashaka hasa wanapoona taarifa kwenye mitandao na vyombo vya habari au kusikia kutoka kwa watu kuhusu janga hili, wazazi wana jukumu kubwa la kuwaelimisha watoto na kuwapa habari sahihi kuhusu ugonjwa huo na namna ya kujikinga ikiwemo kutulia nyumbani na kuacha kuzunguka hovyo mitaani.

Siku za hivi karibuni nimeshuhudia watoto wakizunguka mitaani na wengine wakicheza huku na kule hali ambayo kisaikolojia inajulikana kabisa, wao kutojua mipaka.

Wazazi na walezi, na jamii kwa ujumla ni jukumu lenu kuhakikisha watoto wanabakia ndani katika kipindi hichi ambacho hawaendi shule ili juhudi za serikali kupambanana na virusi vya corona iwe na tija.

Shule zimefungwa kwa ajili ya kulinda watoto , kuondoa Misongamano hivyo sasa wazazi na walezi hawana budi kulinda watoto wasitoke hovyo majumbani kwao na kuwaozesha muda wa kujisomea , kutafakari na kupumzika.

Wazazi lazima tutambue kwamba kama watoto watapata corona itakuwa ni hekaheka kubwa na kuingizana katika majaribu kati yetu, watoto na serikali.

Nioanavyo mimi ni muhimu wazazi au walezi kuchukua hatua madhubuti za kuwabana watoto na wakati huo huo kuwafundisha namna ya kujikinga na maambukizi ikiwamo matumizi ya maji na sabuni katika

MAPEMA mwezi huu vyama mbalimbali vya siasa nchini, vimepuliza kipenga ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi