loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaopata mimba shuleni wapewa utaratibu mwingine

SERIKALI imesema wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito shuleni hawataendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu, badala yake wataendelea na masomo kwa utaratibu mwingine tofauti ikiwemo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi Stadi (VETA).

Hayo yalibainishwa jana na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi, alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha Star Tv katika kipindi cha mada ya ‘Ahadi na Uwajibikaji.’ Katika kipindi hicho, Dk Abbasi alikuwa akipangua hoja zilizokuwa zikitolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo.

Nondo alidai kuwa Kiongozi wao wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na Asasi za Kiraia waliandika barua Benki ya Dunia (WB) kuomba isitishe mkopo wa fedha kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwa fedha hizo zingetumika kutoa elimu kwa kuwabagua watoto wa kike waliopata ujauzito shuleni. Kutokana na madai hayo ya Nondo, Dk Abbasi alisema kuwa suala la wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo halikuanza leo, bali ni msimamo wa Serikali kwa miaka yote. Dk Abbasi alisema Serikali iliweka mifumo ya elimu mbadala kwa wanafunzi wanaopata ujauzito.

“Mtoto wa kike aliyepata ujauzito hajanyimwa haki ya kusoma, wataendelea na masomo kwa utaratibu mwingine tofauti na ule rasmi ikiwemo vyuo vya Maendeleo ya Jamii na VETA,” alisema Dk Abbasi.

Kuhusu mkopo wa elimu wa zaidi ya shilingi trilioni moja ulioidhinishwa na Benki ya Dunia hivi karibuni, alisema mkopo huo unaunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuinua elimu kwa shule za sekondari nchini.

Kwa mujibu wa Dk Abbasi, mkopo huo utawanufaisha wanafunzi zaidi ya milioni sita kwa mwaka kwa kuwajengea mazingira bora ya elimu, lakini pia sehemu ya mkopo huo itaimarisha mifumo na mazingira ya kumfanya mtoto wa kike asipate ujauzito ikiwemo kujenga shule na mabweni.

Akizungumzia mikopo ya elimu ya juu alisema awali ilikuwa ikitolewa kwa wanafunzi wa shule za serikali wenye ufaulu wa daraja la kwanza, lakini Serikali ikapanua wigo na kwa sasa wanafunzi wa shule binafsi pia wanapata mikopo.

Alifafanua kuwa wanafunzi wanaosoma katika shule za kulipia ambao wazazi au walezi wao wamefariki dunia wanapatiwa mikopo na Serikali kama wakiwa na uthibitisho wa vyeti vya vifo.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera na Mwanahija Said, Udom

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi