loader
Mchezaji Bayern apewa adhabu

Mchezaji Bayern apewa adhabu

KLABU ya Bayern Munich imempiga faini mchezaji wake, Jerome Boateng baada ya beki huyo ku- vunja amri ya serikali ya kujifungia ndani baada ya kuondoka hapa na kwenda kumtembelea mtoto wake mgonjwa.

Katika taarifa yake, Bayern imesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikiuka taratibu zilizowekwa na klabu baada ya kwenda mbali na makazi yake bila taarifa. Bavaria ni Jimbo la kwanza Ujerumani kuweka utaratibu wa watu kujikarantini katika jitihada za kujaribu kupambana na mlipuko wa virusi vya corona.

Boateng alisema anauheshimu uamuzi huo, lakini aliuita kuwa ni `majanga’. “Najua kuwa ilikuwa makosa kutoka bila ya kuutaarifu uongozi wa klabu kuhusu safari yangu hiyo, lakini wakati wote akilini yangu yote ilikuwa ilimfikiria mtoto wangu,”alisema Boateng alipozungumza na gazeti la Ujerumani la Bild. “Hakuwa katika afya nzuri.

Wakati kijana anapopiga simu kwa baba yake, bila shaka bado nitaenda, sijui muda gani. “Kwa ajili yake nakubali kabisa adhabu yoyote; kikubwa ni mtoto wangu huyo.

“Nataka kumuona baba ambaye hakwenda kumuona mtoto wake wa kiume, ikiwa kuna adhabu lazima kutakuwa na adhabu kwa hilo. Naiheshimu adhabu hiyo. Na nilihuzunika.”

Hata hivyo, Bayern haikuweka wazo faini hiyo lakini imesema kuwa itachangia katika hospitali za Munich. Katika taarifa yake, klabu hiyo ilisema: “Mwongozo unaohusu tabia za wachezaji FC Bayern katika hali ya sasa pamoja na maelekezo ya serikali ya Bavaria kuhusu uzuiaji wa kutembea ovyo na kuhusu mapendekezo ya mamlaka za afya. “FC Bayern wanaamini kuwa klabu ndio inatakiwa kuwa mfano wa uwajibikaji.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4fa1d9c373ac26d64f439e03943b89f2.jpg

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, ...

foto
Mwandishi: MUNICH, Ujerumani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi