loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kairuki: Serikali inasikiliza na kutatua kero za wawekezaji

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angela Kairuki amewahakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea kukutana na wawekezaji na wafanyabiashara ili kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitatua kwa wakati.

Sambamba na hilo, amesema huduma ya Serikali Mtandao ikiwekwa katika huduma ya uwekezaji itapunguza urasimu na gharama za uwekezaji kuwa itakuwa ni chachu kubwa kwa maendeleo ya nchini.

Akichangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu juzi, alisema: “Naomba kwanza ni wahakikishe Watanzania kuwa serikali itaendelea kukutana na wawekezaji na wafanyabiashara ili kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitatua ili kuunga juhudi jitihada za rais na serikali katika kuleta maendeleo ya taifa.”

Kairuki alitoa pongezi kwa Rais Dk John Magufuli kwa namna mbalimbali alizofanya kukutana na wawekezaji wa ndani na nje mara kadhaa na kisha kutoa maelekezo kwa wasaidizi wake akiwemo yeye na watendaji wote ili wahakikishe changamoto za wawekezaji zinatatuliwa ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Alibainisha kuwa Rais kwa uamuzi wake mzuri na makini wa kuliweka jukumu la kusimamia uwekezaji chini ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa umewezesha kupata mafanikio makubwa katika kusimamia uwekezaji.

Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge kuhusu uwekezaji wakati wakichangia hotuba ya Waziri Mkuu, alisema serikali haitachukua muda mrefu kuweka huduma za Serikali Mtandao katika eneo la uwekezaji ili kupunguza urasimu na gharama za uwekezaji na kuwa itakuwa ni chachu kubwa katika juhudi na maendeleo ya nchi.

“Niwashukuru pia TNDC, TIC, TCCIA, TPSF, CTI, Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, CEO Round Table pamoja na mabalozi wetu nje ya nchi ambao wamekuwa na mchango mkubwa kufanikisha uwekezaji na biashara nchini,” alisema Kairuki.

MBUNGE  wa Mkuranga Abdallah Ulega anatarajiwa kufanya ziara ...

foto
Mwandishi: Angela Semaya, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi