loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Urusi yataka mazungumzo juu ya soko la mafuta

MSEMAJI wa Rais wa Urusi, Dmitry Peskov, amesema nchi hiyo imeandaa mazungumzo yaliyolenga kudhibiti soko la mafuta duniani. Peskov aliyasema hayo katika mahojiano maalumu ya televisheni ya Ikulu ya Kremlin.

“Urusi haikuunga mkono kusitishwa kwa mpango wa Jumuiya ya Nchi zinazozalisha Mafuta (OPEC). Rais Putin (Vladimir) yuko tayari kwa mchakato wa majadiliano na hakuna njia nyingine kuweza kudhibiti vyema soko la kimataifa la mafuta,” alisema.

Kwa mujibu wa Peskov, katika hali ya sasa inayoendelea, mshirika wa Urusi, Saudi Arabia, ametoa punguzo na kuongeza uzalishaji wa mafuta hali itakayosaidia maeneo yote ya kuhifadhi mafuta duniani kujazwa mafuta hayo.

“Matangi sasa hayatumiki kwa usafirishaji wa mafuta, lakini kama makopo ya kuelea. Mwishowe tutapata tu bei ya chini kabisa ya mafuta ambayo haina faida kwa nchi yoyote,” Peskov alisema.

Mpango wa OPEC uliokuwa umejikita kwenye makubaliano baina ya Urusi na Saudi Arabia, kwa miaka mitatu uliruhusu kudhibiti bei ya mafuta kwa dola za Marekani 60 kwa pipa, ulisitishwa Machi, 30, mwaka huu.

Mpango huo ulikuwa ni vigumu kuuendeleza kutokana na kutokuwapo kwa makubaliano ya washirika wakubwa wawili. Urusi walishauri mpango huo uendelee kwa masharti yaleyale hadi robo ya mwaka huu na Saudi Arabia ilitaka kupunguza uzalishaji wa mapipa milioni 1.5 kwa siku hadi mwisho wa mwaka.

Kusitishwa kwa makubaliano hayo kulisababisha kushuka kwa kasi kwa bei ya mafuta, ambayo ilizidishwa na kushuka kwa mahitaji ya kidunia kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

WANANCHI zaidi ya ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

JPM kutikisa Arusha kesho

sekunde chache zilizopita John Mhala, Longido

WANANCHI zaidi ya ...

Wakala mwigine wa Chadema afariki Dunia

masaa 9 yaliyopita Rahimu Fadhili

Katibu Mkuu wa Chama ...

Watakiwa kuanzisha mabucha ya wanyamapori

masaa 10 yaliyopita Na Mwandishi Wetu