loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nadharia ya Aristotle katika maadili

HIVI karibuni, tulichambua nadharia ya John Rawls ya mwaka 1971 ambayo imejikita katika haki zinazotokana na ushiriki wa mtu kwenye jamii yake, ili tuweze kuchambua mambo mabaya na mazuri kwa kutumia nadharia hii kama kioo na hatimaye tuweze kupanua zaidi wigo katika kuyatazama maadili ya utumishi wa umma.

Katika toleo hili, tunachambua nadharia ya Aristotle ili tuweze kutambua mambo yapi ni mazuri kufanya, na yapi ni mabaya na hivyo, hatutakiwi kuyafanya kwa kutumia jicho la nadharia hii na kuona nadharia ya Aristotle inaweza kusaidia vipi katika kukuza maadili katika utumishi wa umma nchini.

Kwa mujibu wa Fallis katika chapisho lake la mwaka 2007 lenye kichwa cha habari “Information ethics for twenty first century library professionals,” nadharia ya fadhila (virtous) ya Aristotle ilianzishwa na Aristotle miaka mingi kabla ya Kristo.

Froehlich katika chapisho lake la mwaka 2000 lijulikanalo kama “Intellectual Freedom, Ethical Deliberation and Codes of Ethics”, anasema nadharia ya Aristotle ni moja kati ya nadharia zilizojikita katika fadhila mbalimbali, zikimaanisha kuwa mambo mazuri ya kufanya katika mazingira fulani, ni yale ambayo yangeweza kufanywa na mtu mzuri katika mazingira kama hayo.

Ili tuweze kujua mtu mzuri ni mtu wa aina gani katika nadharia ya Aristotle, tunaweza kuangalia chapisho la Kraut la mwaka 2020 lenye kichwa cha habari “Altruism”. Katika chapisho hilo, Kraut anasema mtu mzuri ni mtu anayetumia uwezo wake wa kutafakari (reasoning) ili kutambua lipi zuri na lipi baya kwa kuzingatia fadhila mbalimbali kama vile haki, ujasiri, ukarimu, utulivu (temperance) na hali ya urafiki.

Kwa kawaida, mtu mzuri anaongozwa na tafakuri badala ya hisia kama vile chuki na hasira katika kutambua mambo mazuri na kuyafanyia kazi. Hisia kama vile hasira zinaweza kushusha uwezo wa mtu kufanya mambo kwa kuzingatia tafakuri ya kina na hivyo kushindwa kubaini zuri na baya kwa wakati huo. Hata hivyo, siyo kila kitu kinachofanywa na mtu mzuri katika nadharia ya Aristotle ni kitu kizuri na ndiyo maana Froehlich anasema kuwa, nadharia ya Aristotle inasisitiza kuwa katika hali ya kawaida, jambo moja zuri halimfanyi mtu kuwa mzuri na jambo moja baya haliwezi kumfanya mtu kuwa mbaya.

Richter katika chapisho lake la mwaka 1992 lenye kichwa cha habari “Combating Corruption,” anabainishwa kuwa katika nadharia ya Aristotle, msisitizo upo kwenye kujenga tabia njema (moral character) ili kuwa na watu wazuri. Kwa jumla, kwa mujibu wa nadharia ya Aristotle, Cohen na Eimicke katika chapisho lao la mwaka 1995 lijulikanalo kama “Ethics and the Public Administrator” wamebainisha kuwa kujenga tabia njema miongoni mwa watoto ni jambo muhimu sana katika mchakato wa kujenga tabia njema kwa watu wazima.

Kwa maana hiyo, Kraut anabainisha waziwazi kuwa kwa kuzingatia nadharia ya Aris- totle, kujenga tabia njema kwa watoto ni muhimu sana katika kuwajengea mazoea mazuri (habits) ili baadaye iwe rahisi kwao kujijengea hekima zaidi pale uwezo wa kutafakari unapokuwa umejengea zaidi hususan katika kipindi cha ukubwani.

Kuna faida kubwa zinazotokana na matumizi ya tafakuri ili kubainisha mambo mazuri ya kufanya kwa kuzingatia fadhila (virtous) mbalimbali. Kwa mfano, Kraut anasema kwa mujibu wa nadharia ya Aristotle, hali njema ya mtu inatege mea sana uwezo wa mtu huyo kutafakari, ili kuweza kubainisha mambo mazuri kwa kuzingatia fadhila mbalimbali kama vile haki, ujasiri na ukarimu.

Kwa mfano, mtu mwenye mazoea ya kusaidia wengine tangu utotoni na baadaye akiwa mtu mzima akawa amejenga uwezo mkubwa wa kutafakari katika jitihada za kutambua uzuri wa kusaidia wengine kwa lengo la kusaidia tu na kuwanufaisha walengwa, atafaidika na maisha ya aina hiyo.

Vilevile Kraut anabainisha kuwa, kwa mujibu wa nadharia ya Aristotle, hali njema ya jamii nzima inategemea na nia ya baadhi ya watu kuishi maisha mazuri kwa maana ya kuwafanyia wengine mazuri, kwa lengo la kuwanufaisha hao wengine kama vile kuwafanyia watu wengine ukarimu.

MENO meupe na safi ni moja ya vitu vinavyoongeza mvuto ...

foto
Mwandishi: Alfred Nchimbi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi