loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sherehe Pasaka zizingatie usalama wa familia

LEO Wakristo duniani wanasherehekea sikukuu ya Pasaka kufufuka Yesu Kristo, ambapo kama ilivyo desturi ya watanzania bila kujali dini husherehekea pamoja kwa namna mbalimbali.


Mwaka huu, sikukuu hii imekuwa tofauti kuanzia katika utaratibu wa Ibada na hata katika ununuzi wa mahitaji mbalimbali, ikiwemo nguo na vyakula ambapo imeonekana kasi ya ununuzi wa mahitaji ni ndogo kutokana na athari ya mlipuko wa virusi vya corona.

Kutokana na hali hiyo jamii inalazimika kukubaliana na hali halisi kwani virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (COVID-19) umebadili mtindo wa maisha kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na mazingira ya ugonjwa huo, wanawake kama wasimamizi wakuu wa familia ni vema kuwa makini katika kusherehekea sikukuu hii ili kulinda familia na kusaidia kuepuka maambukizi kwa kuhakikisha wanafamilia wote wanaepuka misongamano isiyo ya lazima na kuwazuia kutoka nje ya nyumbani.

Ni vema kuchukua hatua kuanza siku na ratiba maalumu ya kwenda kanisani kwa wale walio wakristo lakini pia kuandaa namna familia zitakavyokaa na kusherehekea majumbani mwao kwa siku nzima ikiwa ni pamoja na kuandaa eneo la kukaa familia kwa pamoja na kuandaa chakula cha familia kulingana na uwezo.

Ni vema kwa ajili ya watoto kama una uwezo kuwapikia chakula kizuri na vinywaji na hata vitu vidogo vya kuwafurahisha ili kutowapa tamaa ya kwenda madukani au maeneo mengine ya kutembea.

Katika hili, si lazima kufanya mambo makubwa ambayo hayakidhi uwezo bali kuandaa chakula cha kawaida huku familia ikihakikisha sikukuu haiharibu mipango mingine ya familia kwani hakika ugonjwa huo umekuwa na changamoto mbalimbali za kifedha.

Ni vema kuweka akiba katika sikukuu na kuepuka kutumia fedha nyingi wakati huu bali kuhakikisha zinatumika kwa wastani ili kuhakikisha familia inafurahi lakini hakuna majuto baada ya sikukuu.

Hakika ugonjwa huu ni hatari kwa maisha ya watu hivyo haitakiwi kufanya mzaha kwa starehe ya siku moja ambayo unaweza kukaa nyumbani na familia na kufurahi na siyo lazima kutoka nje na kwenda maeneo mbalimbali.

Kwa kutambua madhara ya ugonjwa huu, polisi katika mikoa mbalimbali wameshatoa tahadhari ya kuepuka misongamano nyakati za sikukuu hii ikiwemo jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwataka wananchi kuepuka misongamano, uhalifu, vurugu na kwenda maeneo ya fukwe na kwenye baa. Ili kuepuka maambukizi ya virusi hivi, ni vema kuhakikisha tunafuata sheria na taratibu kwa wanaoenda kanisani kuhakikisha hatua zote stahiki zinafuatwa na baadaye kuelekea nyumbani.

Hakuna sababu ya wanawake kutuma watoto maeneo mbalimbali au kuwachukua na kwenda kutembea kwa ndugu au marafiki kwa ajili ya usalama wa afya za familia zetu ni vema kukaa nyumbani.

Ni lazima kukubali kuwa sikukuu ya mwaka huu iko tofauti na miaka mingine kwa kujilinda na ugonjwa huu ni lazima kwa wale wasiozoea kusherehekea nyumbani kufanya hivyo.

Hata kwa akinababa au wanawake wanywaji ni vizuri kwa kuzingatia kanuni za afya kununua vinywaji na kunywea nyumbani na siyo kutoka na kwenda baa ambapo unaweza kupata maambukizi na kuleta athari kwa familia nzima.

MENO meupe na safi ni moja ya vitu vinavyoongeza mvuto ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi