loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Janga la corona: uchumi duniani kutikisika

HALI ya uchumi duniani inaonekana kuwa itakuwa mbaya baada ya janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona kumalizika. Hayo yalibainishwa na Msemaji wa Ikulu,Dmitry Peskov wakati akihojiwa na vyombo vya habari nchini Urusi.

“Leo au kesho, virusi vya corona vitadhibitiwa na labda havitaondoka moja kwa moja. Halafu tena masuala ya uchumi yataendelea, je kinachoendelea sasa athari zake zitaonekana kwenye uchumi? Nawaambia ndio, hali itakuwa mbaya,” alisema Peskov.

Alieleza kuwa baada ya ugonjwa huo, hali mbaya ya uchumi itaendelea duniani kote kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu. “Kwa kweli dunia itapitia kipindi kigumu,” alisema msemaji huyo wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwezi Machi na Kamisheni ya Ulaya ya ukuaji wa uchumi unatarajiwa kushuka kwa asilimia moja. Shirika la Fedha Duniani (IMF) linatarajia hali mbaya zaidi mwaka huu kutokana na kuwepo kwa janga hilo la covid 19.

CHINA imezionya nchi tajiri duniani zinaounda ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi