loader
Wanyama ataja sababu za kusaini Montreal

Wanyama ataja sababu za kusaini Montreal

KIUNGO wa kimataifa wa Kenya aliyekuwa anacheza Tottenham Hotspurs ya England, Victor Wanyama amesema Thierry Henry ndiye aliyemsaidia kujiunga na klabu ya Montreal Impact ya Ligi Kuu ya Canada.

Wanyama ambaye aliondoka Tottenham kwa kumwomba kocha wa timu hiyo Jose Mourinho kutokana na kukosa nafasi ya kucheza, aliamua kujiunga na MLS licha ya kuwa ya kutakiwa na klabu za Hispania na Italia. Wanyama alisema aliyemsaidia kwenda Montreal ni kocha wa timu hiyo Thierry Henry lakini pia aliwauliza wachezaji wenzake wa kama Bojan Krkic ambaye anachezea timu hiyo.

”Wa kwanza kunishawishi ni Thierry Henry ambaye aliiweka wazi kabisa ni kiasi gani ananihitaji kucheza Montreal, aliiuza Montreal kwangu kirahisi sana kwa kuisifia pili niliongea na Luis Binks, ambaye alikuwa akicheza Tottenham, Sapher Taider niliyewahi kucheza naye Southampton na Bojan Krkic wote waliniambia hii ni sehemu sahihi,” alisema Wanyama Wanywama amekaa miaka mitatu na nusu Tottenham na amecheza mechi 97, lakini jeraha la muda mrefu msimu uliopita lilimfanya ashindwe kurudi kwake.

“Nimekuja hapa kupata mahali pa raha tena, kucheza mpira,” “Nawapenda Spurs lakini ilikuwa ngumu. Niliumia muda mrefu, lakini nilirudi na nguvu.

“Sikujiondoa, hata kama sikuwa katika timu, lakini niliendelea kuambiwa nitapata nafasi. Kilichonikatisha tamaa nilijitahidi kupata nafasi lakini sikupata, ningeuliza kucheza kwenye kikosi cha U 23 kupata mkali lakini niliambiwa hapana.

“Nilikuwa kama yai lililovunjika, hata nilipopata michezo ilikuwa ngumu kuwa kwenye kiwango changu, kwani nilikuwa na dakika chache katika kujiandaa,” alisema Wanyama.

Baada ya Mauricio Pochettino kuondoka Tottenham baada ya timu kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu ya Seria A na kuja Jose Mourinho, Wanywama alikuwa na matumaini mabadiliko ya makocha yatakuwa na athari chanya kwake.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f8cada02b50889b06da95c2550b3fd22.jpg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi: MONTREAL, Canada

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi