loader
Makonda- Wananchi Dar lazima wavae barakoa

Makonda- Wananchi Dar lazima wavae barakoa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaagiza wananchi wote wa jiji hilo kuvaa barakoa kuanzia jumatatu wakati wanapokwenda kufanya manunuzi yoyote huku akitaka biashara zote kuanzia siku hiyo kufanyika kwa mfumo wa kununua na kuondoka ‘take away’ ili kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

Akizungumza jijini Dar es Slaam jana, Makonda amesema bila kujali kuwa wananchi hao wana fedha au hawana fedha kwa ajili ya kununulia barakoa hizo ni lazima wahakikishe kuwa wanazivaa kwani wanaweza kuzitengeneza kwa kutumia leso au khanga na kuzivaa pale wanapokwenda kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali sokoni au mahali pengine popote.

“Anayekwenda eneo la manunuzi yotote lazima awe amevaa barakoa (mask), ununue, ukate leso, ukate kanga lazima uwe umevaa, pia kuanzia Jumatatu biashara zote zifanyike katika mfumo wa ‘take away’ ukienda sehemu nunua ondoka, lazima pia kuwe na hatua mita mbili kati ya muuzaji na mnunuzi,” alisema Makonda.

Aidha aliwataka wenye masoko kutumia mfumo mbadala wa kusimamia masoko yao ili kujikinga na corona ikizingatiwa kuwa ugonjwa huo hatari hauonekani kwa macho hivyo mtu yoyote anaweza kuambukizwa wakati wowote kutokana na mazingira anayokuwepo.

Aidha licha ya serikali kuwagiza wauzaji wa barakoa hizo kushusha bei , imebainika kuwa baadhi ya maduka yanauza barakoa hizo kuanzia Sh 2000- 2500 hivyo kuwawia vigumu wananchi wengi kumudu gharama hiyo hivyo kulazimika kufuata ushauri wa Makonda wa kutumia leso au vipande vya khanga kutengeneza barakoa hizo.

Kulingana na kanuni za uvaaji wa barakoa, mtu anapaswa kuivaa barakoa hiyo kwa muda wa saa nne pekee hivyo kumlazimu kutumia barakoa nne kwa siku sawa na kiasi cha Sh 8000 hadi 10,000 kwa siku, hali inayomuwia vigumu kumudu gharama za ununuaji wa barakoa hizo.

Baadhi ya wananchi walishauri wauzaji wa barakoa hizo kushusha walau zifikie Sh 500, bei iliyokuwa ikitumika hapo awali kabla ya kuibuka kwa ugonjwa wa corona ili kuwawezesha wananchi wengi kuzimudu, wakisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo kutawawezesha wananchi wengi kujikinda dhidi ya maambukizi.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile kusema kuwa Wizara inamalizia mchakato wa namna sahihi ya utengenezaji wa barakoa zinazofaa kuvaliwa na wananchi kama njia moja wapo ya kujikinga na virusi vya Corona.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e7367a58a5baf354820824ee0756eb78.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi