loader
Wananchi kulipwa bil 5.2/- mradi gesi asilia

Wananchi kulipwa bil 5.2/- mradi gesi asilia

SHIRIKA la Mafuta la Taifa (TPDC) linatarajia kuwalipa wakazi 693 wa mitaa ya Likong’o na Mto Mkavu katika manispaa ya Lindi Sh bilioni 5.2 mwezi ujao kwa ajili ya kupisha mradi wa kuchakata gesi asilia (LNG).

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk James Mataragio ameyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari, viongozi wa serikali ya mkoa, wilaya, na kueleza kuwa fedha hizo zilitolewa na serikali kupitia shirika hilo.

Dk Mataragio amesema wakati huu maandalizi ya malipo yanafanyika na mpaka Mei zitakuwa zishatolewa kwa wakazi hao.

Alisema kwa sasa kinachotakiwa wakazi hao kufungua akaunti zao ili fidia zilipwe kupitia benki. Alisema ifikapo Mei 17, mwaka huu itakuwa washalipwa fedha hizo na wanaamini wakazi hao watakuwa wamekwisha kufungua akaunti zao benki.

“Hivi sasa mamlaka itakuwa inatoa elimu kwa jamii kuwa wafahamu mradi wao wa kuchakata gas asilia upo, na kazi inaanza kuanzia kuwalipa fidia zao, kipindi hiki,” alieleza.

Amesema sasa yanafanyika mazungumzo ya pili juu ya mikataba baina ya wadau kampuni za Shell na Equinor Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema jamii na waandishi wa habari wafahamu kuwa mradi wa kuchakata gesi asilia upo.

“Haiwezekani serikali itoe shilingi bilioni 5.2 kwa fidia kwa wakazi 693 kuwa mradi hakuna, bali upo jamii na wananchi wafahamu kuwa mradi wao wajiandae kuupokea,” amesema Zambi.

Amesema kinachotakiwa hivi sasa kuwa wananchi wafungue akaunti zao tayari kwa malipo hayo bila kuchelewa ili kupisha mradi kuanza kwa wakati uliopangwa.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga aliwatahadharisha wananchi hao kuwa wanapopata fedha hizo wakumbuke kujenga nyumba sio kutumia bila mpangilo.

Alisema wananchi watapatiwa elimu ya kutosha na wasimamiwa na mamlaka kwa kuwapatia makazi kwa kupewa viwanja vilivyopimwa na halmashauri ya manispaa yao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a52383b6f9acc80449da10b3e41d0a6f.jpg

UKOSEFU wa elimu ya biashara, uthubutu na ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi