loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watalaamu wafafanua njia bora za kujifukiza

WATAALAMU wa afya wamefafanua njia bora za kujifukiza na kutumia viungo asili kwenye chai ili kujikinga na virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid-19).

Wakizungumza na gazeti hili, wataalamu hao walisema jamii inapaswa kufuata njia sahihi za kujifukiza ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kusababishwa na kujifukiza.

Mkurugenzi wa Tiba Asili katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dk Joseph Otieno alisema kujifukiza ni tiba ambayo imekuwa ikitumika miaka mingi na baadhi ya familia hasa katika maradhi ya mfumo wa hewa, kuziba pua, kuwashwa koo na kuumwa kichwa.

Dk Otieno alisema kwa hali ilivyo sasa ya maambukizi ya corona sio rahisi kwa mtu kujigundua kwa haraka kama umepata maambukizi au la na kutokana na uwezo mdogo wa kukabili janga hilo ni muhimu watu kutumia mimea ya kawaida katika kujifukiza angalau mara moja au mbili kwa mwezi kama huna dalili zozote.

Aliongeza kuwa kama tayari una maambukizi basi ujifukize mara tatu kwa siku asubuhi mchana na jioni kwa muda wa dakika tano au 10 kutokana na mtu anavyoweza kuhimili.

Mimea sahihi kujifukiza Dk Otieno alisema tangu wananchi wasikie tangazo la Rais Dk John Magufuli la kushauri watu kutumia njia mbali mbali ikiwemo ya tiba asili ya kujifukiza kujikinga na ugonjwa wa corona, watu wamekuwa wakichanganya mimea mingi kwa wakati mmoja na kujifukizia kitu ambacho sio sawa.

“Mtu changanya magome, anachanganya majani mengi, muarobaini, mpera, mkaratusi na majani mengine mengi hii sio sawa, katika tiba unavyochanganya sio kuwa unaongeza thamani, ni kwamba mchanganyiko mmoja unaweza kuua nguvu ya mmea mwingine ukaua nguvu ya dawa au ukazidisha nguvu ya dawa na ikawa kali na ikaleta madhara,” alisema Dk Otieno.

Alisema mimea inayofaa kwa matumizi ya kujifukiza ni mchaichai, mkarutusi na mfumbasi kwani tayari ilishafanyiwa tafiti na ina machapisho. Alisema mimea hiyo ina vitu muhimu ambayo ukiweka kwenye maji ya moto na kuvuta mvuke wake usaidia kusafisha njia ya hewa.

“Mchaichai, mkaratusi, mfumbasi mdogo, mfumbasi mkubwa, majani yake yakiwekwa kwenye kwenye maji ya moto yana vitu muhimu ambavyo ubebwa na mvuke ambavyo ukivuta ukiwa umejifunika basi uingia kwenye mfumo wa upumuaji na kusafisha,” alisema Otieno.

Akitolea mfano majani ya mchaichai, alisema ukiyachemsha mafuta yake yanapanda na mvuke ambayo ni mazuri na yanasaidia mfumo wa upumuaji, na pia unaweza kuyatumia kwa kupikia chakula, au hata kupaka kwenye ngozi.

Kanuni za kujifukiza Dk Otieno alisema kitaalamu inashauri angalau mtu atumie mmea mmoja, au miwili katika kujifukiza kwa mgonjwa anashauriwa ajifukize kwa dakika tano hadi 10 inategemea na uwezo wa mtu kuhimili mvuke na pia ajifukize kutwa mara tatu, asubuhi mchana na jioni kwa wiki mbili.

“Mtu akiona amefikia kwenye hali nzuri anaweza kufanya mazoezi na haku kohoa basi ujue mapafu yako yapo vizuri, unaweza kuanza kujifukiza mara moja au mbili kwa mwezi,” alifafanua.

Viungo vya chai kukabili corona Dk Otieno alisema kama mtu ni mzima na hana dalili za ugonjwa wa corona ni vema kupendelea kunywa chai yenye viungo vya tangawizi, pilipili manga na mdalasini katika chai na kunywa asubuhi na jioni. Alisema chai hiyo unaweza kuongeza kwa kuweka ndimu au limao kama mtu hana tatizo la vidonda vya tumbo kama ana tatizo hilo basi asiweke ndimu wala limao.

“Kwa mtu aliyeugua akae na chupa ya chai pembeni, kila baada ya dakika 10 awe anakunywa chai hii kuhakikisha koo halikauki na hii itamsaidia sana,” alisema Dk Otieno.

Alisema unywaji wa chai hiyo husaidia kuongeza nguvu ya kinga ya mwili dhidi ya magonjwa, huboresha mfumo wa umeng’enyaji chakula, hupunguza maumivu, na kuongeza uwezo wa utambuzi wa mtu. Alisema pia husaidia kulinda moyo, kudhibiti kisukari, kupunguza kiwango cha wasiwasi na kuboresha ubora wa ngozi.

Madhara Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (Tramepro) cha Dar es Salaam, Bonventura Mwalongo alisema jukumu la kujifukiza linahitaji utalamu na ungalifu, kwani mtu anaweza kutumia mimea isiyo sahihi na kuleta madhara.

“Anayetumia kujifukiza anapaswa kufuata maelekezo kwa watu wenye utalamu sio kukimbilia kuvunja miharobaini, mibani, mikungu, milimao na mengine bila kufuata maelekezo ya watalamu,” alisema Mwalongo.

Alisema kujifukiza sio chanjo ya corona, lakini ni ‘component’ inayoweza kusaidia katika matibabu ya ugonjwa huo. “Kujifukiza ni kuzuri bila kujali changamoto ya kiafya au la angalau fanya hivyo mara mbili au tatu kwa mwezi ili kuweka sawa mfumo wako wa hewa,” alisema Mwalongo.

Hata hivyo, alisema wananchi wanapaswa kuwa wangalifu kwani kitu chochote kinapotumika bila uangalifu huleta madhara, na kuwatadharisha wale wanaojifukiza kila siku wapo hatarini kupata magonjwa ya ini, magonjwa ya mfumo wa hewa ikiwemo kushindwa kutambua harufu ya kitu, mdomo kukosa ladha na mwili kuvilia.

NIMR yatoa neno Nayo Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imewataka wananchi kutochanganya mimea zaidi ya minne katika kutengeneza tiba joto au mvuke wa kujifukiza kwa ajili ya kujitibu ugonjwa wa Covid-19. Ikiwa wananchi watatumia mimea zaidi ya minne, kuna uwezekano mkubwa kwa dawa hizo kuanza kupambana zenyewe katika utendaji badala ya kumsaidia mgonjwa.

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana ofisini kwake Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya alisema wanapendekeza aina tatu za mchanganyiko wa mimea tiba kutengeneza joto tiba au mvuke. Aliutaja mchanganyiko wa kwanza wa mimea ambayo wananchi wanaweza kuutumia ni mchanganyiko wa majani ya mkaratusi, majani ya kivumbasi au kashwagala na majani ya mchaichai.

Aina ya pili ni mchanganyiko wa majani ya mchaichai, karafuu, tangawizi iliopondwapondwa na majani ya mlimao. Aliutaja mchanganyiko wa tatu kuwa ni majani ya mwarobaini, majani ya mpera, mchaichai na majani ya mlimao.

Kwa mujibu wake, tiba joto hiyo au mvuke ni muhimu kwani inasaidia kuongeza kinga ya mwili, kufungua njia ya hewa na kukirarua kirusi cha corona kama bado kiko kwenye njia ya hewa na hakijaingia kwenye mapafu.

Alisema tiba ya kujifukiza haisaidii kama tayari kirusi cha corona kimeshaingia kwenye mapafu, hivyo mgonjwa anatakiwa kupewa matibabu mengine ikiwemo antibiotic.

Joto nyuzi 50-70 “Joto la mvuke linatakiwa liwe kati ya nyuzi 50 hadi 70, likizidi linaweza kuumiza njia ya hewa, mtu anatakiwa avute mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni, watu wazima wavute kwa dakika nane hadi kumi na watoto kuanzia umri wa miaka saba wavute kwa dakika mbili hadi nne, watoto chini ya miaka saba hawaruhusiwi kutumia tiba hii,” alisema Profesa Mgaya.

Kwa kuwa mvuke una kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni, alisema watu wenye matatizo ya kupumua hawapaswi kutumia tiba hiyo kwani wanaweza kupoteza maisha, pia wanaotumia wasijifukize wakati sufuria iko kwenye jiko la mkaa bali iwekwe chini au mahali pengine kwa kuwa mkaa hutoa hewa yenye sumu hatari kwa binadamu.

Kuhusu maandalizi ya dawa hiyo, Profesa Mgaya alisema hatua ya kwanza ni kuchemsha maji ya lita tano au kumi hadi yachemke, kisha yawekwe majani na kuyafunika na kuyachemsha kwa dakika tano tu.

Alisema dawa ikichemshwa kwa zaidi ya dakika tano inakuwa imepikwa na haifai kwa tiba kwa sababu virutubisho muhimu vinakuwa vimepotea kwa njia ya mvuke.

Alisema wakati wa kujifukiza mtu anaweza kujifunika kwa blanketi au shuka au taulo zito ili mvuke usipotee, na baada ya kujifukiza muhusika asipewe maji baridi ya kunywa kwani ataharibu tiba bali apewe glasi ya maji ya moto au chai.

Kuhusu kipimo cha dawa hizo, alitoa kipimo kwa mchanganyiko wa kwanza tu ambapo mtu anatakiwa atumie gramu 50 za majani ya mkaratusi na gramu 50 za kivumbasi na gramu 20 za mchaichai

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro na Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi