loader
Picha

Shule za msingi, sekondari sasa kufunguliwa Septemba

WIZARA ya Elimu imesema shule za msingi na sekondari zitafunguliwa Septemba, mwaka hu una kuwaondoa hofu walimu na wanafunzi kuwa shule hazitafunguliwa mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na baraza la mawaziri katika kikao chake cha kutathmini mapambano ya kudhibiti virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19. Waziri wa Elimu, Teknolojia ya Mawasiliano na Elimu ya Ufundi, Claudette Irere, alisema taasisi nyingine za elimu zitafunguliwa baada ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuanza masomo.

“Kwa taasisi za elimu tunafahamu kuwa wapo waliobakiza miezi michache kumaliza mwaka wa masomo, hivyo watarejea vyuoni mara baada ya shule za msingi na sekondari kufunguliwa,” alisema.

Alisema walimu wa shule za umma wataendelea kupata mishahara yao ya mwezi kwa sababu wanaendelea kusaidia wanafunzi kupitia mifumo mbalimbali ya mafunzo.

“Kwa walimu wa taasisi binafsi, ambao wameathirika sana wakati huu, tunataka wamiliki wa taasisi hizo kutafuta misaada katika mifuko ya serikali ya kusaidia sekta binafsi ili waendelee kuwalipa walimu wao,” alisema.

Kuhusu wazazi waliolipa ada, Irere alisema hakutakuwa na kurejeshwa ada, kwani janga hilo limeathiri watu wengi na kwamba muda huu mpaka Septemba utatumika kujenga madarasa zaidi ili wanafunzi watakapofungua shule kuwe na uwiano mzuri baina ya walimu na wanafunzi.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: KIGALI

17 Comments

 • avatar
  SALAMU CHACHA
  05/05/2020

  Mimi ni mwanafunzi wa shule ya secondary, kidato cha tatu, tukifungua shule hyo mwezi wa September, tutaendelea na madarasa yetu au mwaka ujao utarudia darasa kwani tumepoteza muda mwingi sana wa kusoma kwa janga hili la COVID-19.

 • avatar
  ASTILIES MUBEZI ABRAHAMU
  06/05/2020

  Serikali ndiyo itakayo toa tamko kama 2narudia mwaka wa masomo au la!

 • avatar
  NYABUYENZE
  06/05/2020

  Comment. IFIKE WAKATI SERIKALI IFUNGUE VYUO,TAHADHARI ZIKICHUKULIWA HAKUTAKUWA NA TATIZO,ILI TUKAMALIZIE MWAKA KWA SEMESTER HII KWA MUDA ULIYOBAKI.

 • avatar
  abdu
  09/05/2020

  Comment kwakweli ham ya kusoma ha2na

 • avatar
  Nindwa nkenyenge
  10/05/2020

  Comment kwa kweli hili ni janga kubwa serikali ndo final saying ju ya hili ,wizara ya afya ikiruhusu shule itabidi turudi

 • avatar
  MAULID
  12/05/2020

  VP KUHUSU SHULE MWAKA HUU WATARUDIA NN MADARASA..?

 • avatar
  Kijanga shigela
  15/05/2020

  Jamani itabid kurudia tu bcoz saiv tumesahau vitu ving sana

 • avatar
  Deo maleck
  15/05/2020

  Comment serikali itoe elimu hasa kupitia mitandaoni ili kuwasaidia wanafunzi wakati wa janga hili la covid-19

 • avatar
  Ibrahim mwitaniji
  16/05/2020

  Comment!,kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi,wanafunzi tukomae2 kama ipo ipo2.

 • avatar
  R@phael masalu jomo
  20/05/2020

  Comment Mamba sec school

 • avatar
  CASTOR BUDEBA SHIJA
  20/05/2020

  Comment napenda kuuliza madarasa 2narudia 2napofungua shule au hapana!

 • avatar
  Salvation Ernest
  21/05/2020

  Jamani shule 2fungue mana janga la korona kidogo limepungua nchini

 • avatar
  Uthman Bin Alliey
  22/05/2020

  Sasa kwa hiyo tunarudia madarasa au inakuwaje?

 • avatar
  HEPMARK
  23/05/2020

  Comment jamani 2rudie masomo mwakani kwan tumesahau vitu vingi sana tunaweza kufeli necta

 • avatar
  RICHARD
  23/05/2020

  Comment jamani tufungue shule mpaka janga litakapo isha kabisa na ningependa turudie vidato mwakani ili tuweze kujiandaa vizuri na mtihani wa taifa (necta).

 • avatar
  Gift Irene
  26/05/2020

  Mimi nimzaz mwanangu anasoma shule ya msing mavurunza kimara ,ndugu zanguni ikibidi Yale madarasa ya mtihani inabidi warudie kama itawezekana Mana watoto wengne kusoma awataki wanasbr mpka shule duuuuu Corona wew sjui ultumwa Mana umetuyubsha ata waksema wanafnz waende twshe. Mmango kachu atuna hata mbun

 • avatar
  Daniel manang'oi
  27/05/2020

  Comment: Hatuna budi kurudia darasa, cha msingi wanafunzi tufanye marudio kwani huwaga tu 80% inakuwa nyuma kwa NECTA. corona isiturudishe nyuma. Kufunguliwa kwa shule tusubiri corona ishe! tusije kuangamiza taifa la kesho! nko mondul- call 0626428081

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi