loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mourinho alilia Real ilipofungwa na Bayern

KOCHA Jose Mourinho amesema alilia sana baada ya Real Madrid kufungwa na Bayern Munich katika mechi ya nusu fainali ya kuwania Kombe la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 2012.

Bayern Munich ilimtoa machozi Jose Mourinho walipoifunga Real Madrid na kuitoa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, miaka nane iliyopita. “Usiku ule ndio wakati pekee nimewahi kulia,” alisema Mourinho katika mahojiano na gazeti la michezo la Hispania, Marca.

“Nakumbuka vizuri sana, mimi na Aitor Karanka (msaidizi wa Mourinho), tuliegesha gari mbele ya nyumba yangu, tukilia.” “Hali ilikuwa ngumu sana kukubali kipigo hicho kwa sababu msimu huo wa mwaka 2011-12 tulikuwa timu bora Ulaya.”

Wiki iliyopita imetimia miaka minane tangu Mourinho alipofikisha mwisho wa ubabe wa Pep Guardiola katika Ligi ya Hispania, La Liga kwa kushinda ligi hiyo na rekodi ya alama 100.

Lakini Mourinho pia alikuwa na fursa ya kushinda taji ambalo lingekuwa la 10 la mabingwa wa Ulaya, lakini wakapoteza mechi yao na Bayern Munich kwa penalti, huku Cristiano Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos wakikosa penalti.

“Hilo pia ni soka, Cristiano, Kaka na Sergio Ramos, wote ni miamba wa soka, hilo halina ubishi kabisa. Lakini pia hao ni binadamu,” alisema Mourinho.

Akikumbuka kuhusu kushinda taji la La Liga, Mourinho alisema: “Hayo yalikuwa mabao yangu matatu, tukiweka kando Ureno.

Nilitaka kushinda Ligi ya England, Italia na Hispania. Na mimi bado ni kocha pekee niliyefanikiwa kufanya hivyo.” Mourinho kocha raia wa Ureno kwa sasa anafundisha klabu ya Tottenham.

Baada ya siku chache Ozil kutojumuishwa kwenye orodha ya wachezaji ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi