loader
Daraja litakalounganisha China na Urusi lazinduliwa

Daraja litakalounganisha China na Urusi lazinduliwa

WAZIRI wa Ujenzi, Nyumba na Huduma Urusi ameidhinisha uzinduzi wa daraja la kwanza la magari la Urusi na China lililojengwa kwenye mto uliopo mpakani mwa nchi hizo wa Amur.

Daraja hilo ambalo ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2016 na kukamilika Desemba, mwaka 2019, limeunganisha miji miwili ya nchi hizo ambayo ni Blagoveshchensk na Heihe.

“Kampuni ya pamoja ya Urusi na China ilipewa ruhusa ya kufungua mpaka wa daraja hilo. Hili ni daraja la kwanza la gari kati ya Urusi na China. Ruhusa rasmi imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Nyumba na Huduma,” alisema waziri huyo.

Pamoja na idhini hiyo daraja litaanza kutumika rasmi baada ya masharti magumu yaliyowekwa sasa baina ya nchi hizo mbili ya kukabiliana na virusi vya homa ya mapafu, covid 19 kutolewa.

“Kama isingekuwa janga hili la corona, mipaka iliyofungwa daraja lingeanza kutumika lakini sasa ni vigumu kwani hali ya kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huu bado ni mbaya duniani.

Daraja litafunguliwa rasmi baada ya masharti yote kulegezwa au kuondolewa,” alisema. Blagoveshchensk ndio wilaya pekee katikati ya nchi ya Urusi iliyopo mpakani baada ya kuvuka mto Amur kuna mji wa Heihe wa nchi ya China. Daraja hilo linakadiriwa kuwa na uwezo wa kuvusha watu milioni tatu, mizigo yenye uzito wa tani milioni sita na magari 300,000 kwa mwaka.

Aidha, daraja hilo lina urefu wa kilometa moja wakati urefu mpaka mzima ni kilometa 20 zikiwemo kilometa sita za barabara upande wa China na kilometa 13 upande wa Urusi.

Mradi huo uligharimu dola za Marekani milioni 254.9 na fedha hizo zinatarajiwa kurejeshwa ndani ya kipindi cha miaka 16 kupitia tozo itakayotozwa kwa watakaotumia daraja hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4bc652a07e4fdf10b3e037d9d692d113.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi