loader
Mwanamke mwenye umri mkubwa apona corona

Mwanamke mwenye umri mkubwa apona corona

MWANAMKE anayesadikiwa kuwa mwenye umri mkubwa nchini Hispania, amepona ugonjwa wa homa ya mapafu, unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

Taarifa rasmi zinasema Maria Branyas (113) alipimwa na kukutwa na ugonjwa huo Machi mwaka huu nchi ilipoamuru watu wote kutotembea. Baada ya wiki kadhaa akiwa amejitenga, ajuza huyo alipona na kubaki na dalili ndogo.

Mwanamke huyu anatajwa kuwa amepitia majanga mengi mojawapo ikiwa ni homa ya mafua iliyotokea mwaka 1918 hadi 1919; vita ya wenyewe kwa wenye ya Hispania ya mwaka 1936 hadi 1939 na kisha Covid-19.

“Sasa yuko vizuri, inafurahisha, anataka kuongea kuelezea,” binti yake aliandika katika ukurasa wake wa twitter. Branyas alizaliwa nchini Mexico mwaka 1907.

Alizaa watoto watatu ambao mmojawapo hivi karibuni alitimiza miaka 86 na ana wajukuu 11 ambao mkubwa ana umri wa miaka 60. Ana vijukuu 13. Kwa miongo miwili amekuwa akihudumiwa nyumbani katika mji wa Olot.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ed6a410d28928dabb9d0f56cc14080d0.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi