loader
Maseneta Marekani waonya usambaaji wa virusi

Maseneta Marekani waonya usambaaji wa virusi

MASENETA nchini Marekani wameonywa kuwa virusi vitasamba, iwapo nchi itafungua shughuli zake mapema. Daktari wa ngazi ya juu wa magonjwa yanayoambukiza, Dk Anthony Fauci alisema miongozo ya shirikisho ya kufungua tena shughuli za kibiashara isipofuatwa, maambukizi madogo madogo yatageuka mlipuko.

Dk. Fauci alikuwa akizungumza kwa njia ya video na kamati ya seneti, inayoongozwa na Republican nchini Marekani. Alisema pia idadi halisi ya vifo nchini Marekani, huenda ikawa kubwa kuliko idadi rasmi inayotolewa ya vifo 80,000.

Mwito wa daktari huyo uko kinyume na taarifa iliyotolewa na Rais Donald Trump aliyedhamiria kutaka shughuli za kiuchumi zifunguliwe tena. Daktari huyo alikuwa akielezea kuhusu mpango wa kufunguliwa upya kwa shughuli Marekani, baada ya majimbo zaidi ya 12 kuweka amri ya kukaa nyumbani kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Mpango huo unajumuisha awamu ya siku 14, ambazo majimbo yametakiwa kuzizingatia wakati wanaporuhusu kufunguliwa kwa shule na biashara. Majimbo kadhaa ya Marekani yaliyoanza shughuli zao za kiuchumi, yanatajwa kuwa na viwango cha juu cha ongezeko la maambukizi badala ya kushuka.

Alionya inawezekana kusababisha mlipuko, ambao maofisa hawataweza kuudhibiti na kwamba mlipuko wa aina hiyo utarudisha nyuma kufufuka kwa uchumi. Ingawa Ikulu imeweka miongozo ya kufungua shughuli za kiuchumi , ni jukumu la magavana kuamua juu ya namna ya kulegeza sheria za kukaa nyumbani zilizowekwa.

“Bila shaka, hata katika hali nzuri sana, ukipunguza hatua za kudhibiti maambukizi utaona visa vinajitokeza,” alisema Dk Fauchi.

Dk Fauci alisema kuwa kuna chanjo nyingi ambazo zinatengenezwa, lakini hakuna uhakika wa yenye ufanisi . “Tuna nyingi zinazofanyiwa uchunguzi na natumai zitaweza kufikia viwango vinavyohitajika,”alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2c0e0ae00880ee7b8a84a65971e12464.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi