loader
Rais wa Madagascar afafanua dawa yao ya corona

Rais wa Madagascar afafanua dawa yao ya corona

WAG ONJWA wal ioitumia dawa ya mitishamba iliyogunduliwa nchini Madagascar ikwa ajili ya kutibu ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19), afya zao zilianza kuboreka ndani ya saa 24 na kupona baada ya siku 10.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina kwenye mahojiano maalumu kati yake na chaneli ya RFI na France 24 yaliyofanywa hivi karibuni. Waandishi wa habari wa vyombo hivyo waliohusika na mahojiano hayo ni Christophe Boisbouvier na Marc Perelman.

Rais Rajoelina alisema dawa hiyo isiyo na sumu, inayojulikana kama Covid-O rganics au Tambavy CVO , imetengenezwa na mimea tiba ya nchini humo na sehemu kubwa (asilimia 62) ni mmea wa Artemisia.

Rais Rajoelina ambaye alisema hawezi kufichua kanuni ya mchanganyiko wa dawa hiyo kwa sasa, alisema utaratibu wa utengenezajiu wa dawa hiyo, ulizingatia kanuni za kawaida za utengenezaji wa dawa na uangalizi wake. Alisema nchi yake imepeleka dawa katika mataifa mengine ya Afrika, kwa kuwa imeonesha kufanyakazi kwa wagonjwa walioitumia.

“Nataka kuwaambia kwamba wagonjwa waliopona walitumia hii Covid- O rganics (pia tunaiita Tambavy CVO ). Kwa ufupi, afya za wagonjwa waliotumia Tambavy CVO zilianza kuboreka ndani ya saa 24 baada ya kunywa dawa hiyo kwa mara ya kwanza… Hii dawa ni ya asili, isiyo na sumu,” alisema Rajoelina.

Wakati wa mahojiano hayo, Rais huyo alisema nchini mwake kuna watu 171 waliothibitika kuwa na Covid-19, ambao kati yao 105 wamepona. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizochukua dawa hiyo nchini Madagascar.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi alikwenda na wataalamu wa afya nchini humo, kuichukua baada ya Rais Dk John Magufuli kutoa ndege kwenda kuifuata nchini humo.

Awali, mwandishi Perelman alisema Taasisi ya Utafiti ya Malagasy (IMRA) imekataa kuweka wazi mchanganyiko halisi wa Covid-O rganics, kwa kile kinachohisiwa ni kuepuka kuwahiwa na washindani, kabla ya kuwa na haki miliki.

Hata hivyo katika swali lake alisema, kwa kuwa watu wengi wa vijijini hawawezi kufikia dawa hiyo, ingekuwa vyema wakaelekezwa waweze kutengeneza dawa wenyewe na hivyo kujilinda.

“Unaweza kutuambia kilichoongezwa kwa Artemisia, mimea mingine miwili iliyotengeneza Covid-O rganics?,” alihoji. Rais Rajoelina alisema haipaswi kubeza wanasayansi wa Afrika na Madagascar.

“Kuna tatizo gani la Covid-O rganics? Nafikiri tatizo ni kwamba inatoka Afrika. Na hatuwezi kukubali, kupokea kwamba nchi kama Madagascar, ambayo ni nchi ya 63 kwa umasikini duniani, imeweza kutengeneza kanuni na kupata Tambavy CVO kuokoa dunia. L akini hii ni vita,” alisema.

Alisisitiza, “Ninachoweza kusema leo ni kwamba kwa suala la wagonjwa waliopo Madagascar na pia wale waliochukua hizi dawa, kwa kweli Tambavy CVO , tuna uthibitisho kwamba tumewatibu wagonjwa wetu.”

Alisema iwe ni nchi au shirika lolote ikiwamo Shirika la Afya Duniani (WHO ), hakuna kitakachowazuia kusonga mbele, ikizingatiwa kwamba nchi yake ni huru na ipo kusaidia watu wake.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/01826708d2f7381de6d525f451a52736.jpg

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka vijana wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi