loader
Canada sasa yahidhinisha jaribio chanjo ya corona

Canada sasa yahidhinisha jaribio chanjo ya corona

SERIKALI nchini Canada imeidhinisha kufanyika kwa majaribio ya kwanza ya chanjo ya ugonjwa wa Covid-19.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Ottawa mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau (pichani), alisema kuwa Kituo cha Chanjo cha Canada katika Chuo Kikuu cha Dalhouse kimeruhusiwa Idara ya Afya Canada kuanza majaribio ya chanjo hiyo.

“Endapo majaribio haya ya chanjo yatakuwa na mafanikio, tutazalisha na kusambaza hapa nchini; utafiti na maendeleo huchukua muda, na lazima yafanyike kwa usahihi, lakini hata hivyo taarifa hii inatia moyo,”alisema Waziri Mkuu Trudeau.

Trudeau aisema Baraza la Taifa la Utafiti la Canada litafanya kazi na wazalishaji chanjo hiyo muhimu ili izalishwe nchini humo kama majaribio yatakuwa mazuri. Imeelezwa kuwa mpaka juzi mchana, jumla ya wagonjwa 75,770 wa Covid-19 walithibitishwa nchini humo, vifo vikiwa 5,677.

Idara ya Afya Canada imeruhusu kufanyika kwa majaribio 33 ya kusaidia au kutibu ugonjwa wa Covid-19. Mei 12 mwaka huu, Baraza la Taifa la Utafiti la Canada lilitangaza mpango wake wa kushirikiana na Kampuni ya Chanjo ya CanSino Biologics Inc (CanSinoBIO) kwa ajili ya kuendeleza mchakato wa chanjo ya Covid-19.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6fa368bf24b46e4677cb99e4ac67b93c.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: OTTAWA, Canada

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi