loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Ni wakati wa kuvuna matunda ya Kiswahili

MKUTANO wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) uliofanyika Tanzania mwaka jana, ulipitisha azimio la kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi katika jumuiya hiyo.

Ni wakati sasa wa kuvuna matunda ya Kiswahili. Tuanze sasa na sisi wenyewe kukitumia Kiswahili kikamilifu. Na hakika juhudi hizo zimeshaanza hata kabla ya azimio la mkutano wa Sadc.

Itakumbukwa kuwa, Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia mapema mwaka huu ilizindua mitaala ya kufundishia mafunzo ya ufundi (Veta) kwa lugha ya Kiswahili ili itumike kwenye vyuo vya maendeleo ya wananchi vipatavyo 54 kote nchini. Hii ni hatua ya kupongezwa.

Ikumbukwe, duniani hapa, lugha ni nyenzo na silaha muhimu hata kwenye mapambano ya kujikomboa kiuchumi. Kiswahili kama lugha, kinapaswa kiimarishwe kwenye sekta ya elimu na namna ya kuyapata maarifa. Itakumbukwa, hapa nyumbani, Serikali ya Awamu ya Nne ilipata kuzindua sera mpya ya elimu nchini.

Sera hiyo ilitaka elimu ya msingi iunganishwe na sekondari. Na kwamba lugha ya kufundishia na kujifunzia iwe ni Kiswahili, kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu, Bahati njema, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, imekuwa mstari wa mbele katika kukiweka mbele Kiswahili.

Hivyo, kujenga matumaini kuwa, kwa kutumia Kiswahili kwenye elimu yetu, basi tutakuwa na ‘ Elimu Kombozi’ kwa Watanzania. Na kuna waliotutangulia kufanya mapinduzi ya kisera na wamefanikiwa. Tuone hapa mfano wa nchi ya Singapore.

Imeandikwa kuwa, Singapore ‘chunusi kwenye uso wa Malaysia’ ina eneo dogo sana (kilomita za mraba 646 sawa na eneo la jiji la Chicago, Marekani). Idadi ya watu haifikii milioni tano, ambao wamejigawa ki-uzawa; yaani, wa-Hindi, wa-Malay na wa-China.

Zaidi, wamejigawa ki-dini; yaani, wa-Islamu na wa-Budha. Masuala ya siasa, ubaguzi wa rangi au dini hayaruhusiwi kuwa viini zungumziwa na wasanii. Kisiwa cha Singapore kilianza kama kijiji cha wavuvi wachache.

Kilijaa mabwawa ya mbu wengi wenye kueneza ugonjwa wa malaria. Bandari na mandhari ya ufuko wake kulijaa mitumbwi.

Walevi wa madawa ya ‘opium’ walijaa kwenye sehemu walikoishi jamii ya wa- China, ambao walikuwa wakichungulia madirishani na huku wamewaka chakari, mbali ya wacheza kamari na kusheheni biashara ya ukahaba na ushoga (changudoa).

Licha ya sifa hizo mbaya, kisiwa cha Singapore kilikuwa kikigombaniwa kati ya Uingereza na China kutokana na jiografia yake. Waingereza walikitawala kwa muda wa miaka 149 kwa lengo la kukifanya mahali pa biashara na maghala/ soko makubwa kama Hongkong, kwa masoko makubwa ya kikoloni ya kifedha na dhidi ya biashara ya dawa za kulevya chini ya China. Mwaka 1963 kisiwa hicho kilijitawala chini ya Muungano wa Malaya na Majimbo ya Sabah na Sarawak.

Lakini Mungano ulivunjika 1965 kutokana na wa-China na wa-Malaysia kugombana. Vyuo vikuu vilijaa wasomi wa mkono wa kushoto; Wakomunisti waliiingilia vyama vya wafanyakazi; na haikuwa na jeshi la ulinzi. Haikuwa na maliasili na eneo la kuzidi kupanuka; mji mchafu wa kunuka; mifereji ya maji machafu na taka kila mahali; na ajira haba.

Zaidi, ilikuwa ina agiza maji na chakula kutoka nje ili kusaidia lishe nchini, ingawa ilikuwa na nguruwe, matunda na mboga; majitaka yalinuka kila mahali; na ajira haba sana kiasi cha asilimia 14 na wenye manywele marefu kutapakaa kila mahali.

Singapore ilijiuliza maswali mazito: Singapore inaishi katika ulimwengu wa hali gani? Singapore imetoka, iko na inakwenda wapi? Singapore itilie mkazo mafunzo gani mashuleni ili kuweza kufanikisha ndoto ya maisha bora kwa wananchi wake?

Singapore iliamua kujijenga ili kujikomboa kutoka madhambi, majuto na mavune ya miaka mingi kabla ya 1960. Ilipiga marufuku makasino, kamari na kuongeza kodi kwa tumbaku na vinywaji vikali na kudhibiti biashara ya dawa za kulevya.

Ili kudhibiti umaskini na mazoea yasiyo ya maadili mema, serikali ililivalia njuga suala la umasikini. Singapore ilianza kufyeka na kujenga upya bandari na madhari yake, ingawa iliashiria kutambulika kama nchi itakayojiunga na maswaiba wa nchi fukara za dunia ya tatu.

Lakini Singapore ilijinasua kuitwa hivyo. Wafanyakazi walihimizwa kuchapakazi. Leo hii, Singapore ni bandari-ghala (entrêport) kubwa kwa nchi zote za Australia, New Zealand na Asia Mashariki ya Mbali. Biashara ya huko ni kubwa sana; haiwezi kulinganishwa na biashara inayopita Dar es Salaam kwenda nchi za jirani.

Biashara nchini humo ilikuza miundombinu iliyojengwa kwa ajira ya unyonyaji wa mfumo wa manamba (wa-China, wa- Sri Lanka na wa-Hindi).

Wananchi walitokana na mchanganyiko wa mataifa, dini na lugha nyingi, kwa mifano, Waingereza, Wahindi, Wamalaysia, Wachina na Wajapani; dini nyingi, kwa mifano, wa-Budha, wa-Tao, wa- Islamu, wa-Confucius, wa- Kristo na wa-Hindu); na lugha nyingi, kwa mifano, kingereza, kimandarini, kimalaysia na kitamili). Lakini leo hii kuna mataifa matatu makubwa” Wahindi, Wachina na Wamalaysia.

BAADHI ya wanaume tumekuwa na mtazamo ...

foto
Mwandishi: Maggid Mjengwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi