loader
Makonda- Jumapili pigeni shangwe

Makonda- Jumapili pigeni shangwe

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wananchi wote waliokimbia mkoani huo na kwenda mikoani kwa ajili ya kujifi cha kupata maambukizi ya virusi vya corona, kurejea na kufanya kazi.

Amesema Jumapili wiki hii, wakazi wa jiji hilo wajitokeze kwa wingi kupiga kelele katika maeneo mbalimbali ikiwa ni ishara ya kumshukuru Mungu kwa kuishindia Tanzania na maambukizi hayo ya virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (Covid-19).

Makonda alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea daraja la Tanzanite linalopita eneo la baharini, na kusema linatarajiwa kukamilika Oktoba, 2021 na lina kilometa tisa kutoka usawa wa bahari.

Kuhusu kurejea kwa wakazi wa jiji hilo, alitoa wito kwa wote waliokimbia kwa hofu ya maambukizi ya corona kurudi na kufanya kazi kwa bidii huku akiwataka pia wenye hoteli, baa na kampuni mbalimbali kufungua na kuhakikisha kazi zinaendelea kama kawaida.

“Wafanyabiashara na wafanyakazi wote wa Dar, kama una hoteli, baa, kampuni tufungue shughuli zetu tufanye kazi. Wale wote waliokimbilia mikoani kwa ajili ya kusubiri corona ipite warudi watatukuta tuna afya njema na waje tuchape kazi,” alisema Makonda.

Alisema wananchi hao warudi kwenye shughuli za kiuchumi, wasijifungie ndani huku Rais John Magufuli akiwa ameshasema ila waendelee kutekeleza masharti ya wataalamu wa afya, anga limefunguliwa ni muhimu sasa hoteli zifunguliwe na wateja waje na dunia itambua kuwa Rais Magufuli anaongozwa na maono ya Mungu.

Alisema wakazi wa jiji hilo warudi kazini ilmradi wanajua kunawa mikono kwa maji tiririka, kukaa umbali wa mita moja baina ya mtu na mtu, kwani Mungu ameipendelea Tanzania.

Kuhusu siku tatu za maombi ya shukrani, alisema yatafanyika Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hii na kuwataka wakazi wa jiji hilo kila mmoja kupiga shangwe na kelele kwamba Mungu ameishindia Tanzania.

“Katika siku hizo tatu za ibada, siku ya Jumapili iwe ni maalumu kwa kupiga kelele, kama utaenda disko nyumbani piga kelele, toka barabarani piga kelele kama unaenda baharini kuogelea kwa furaha fanya hivyo, Mungu wetu ametushindia na Jumatatu tarehe 25, kazi ziendelee kama kawaida,” alieleza Makonda.

Aidha, aliwataka wakazi wa jiji hilo kuendelea kufanya mazoezi ya mwili kadri iwezekanayo, kwamba iwe asubuhi na jioni kwa kuwa ndio muda wa kujenga mwili na kuuufanya kuwa na afya njema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9a483b3d719c687b036800f57dd39b3d.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi