loader
Picha

Corona yaathiri utoaji haki

SHIRIKA la Msaada wa kisheria la Legal Services Facility (LSF) limesema upatikanaji haki kwa wananchi umeathirika kutokana na kuzuka kwa homa kali ya mapafu ya covid-19 inayosababishwa na virusi vya corona nchini.

Akizungumza na HabariLEO jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala alieleza utekelezaji wa mradi wa ‘Access to Justice’ umeathiriwa na virusi vya corona.

Alisema ni muhimu kwa wadau kutafuta njia mbadala kutekeleza shughuli zao kuwawezesha wananchi kuendelea kupata haki zao zote. LSF inawawezesha wasaidizi wa kisheria zaidi ya 3,700 nchini kuwafikia wananchi kila wilaya na kutoa elimu ya kisheria kutatua changamoto.

Watoa huduma hawa wamekuwa wakitoa elimu katika mikutano mikubwa ya hadhara, bonanza, vikoba, shuleni, sehemu za ibada na maeneo mengi yenye mkusanyiko wa shughuli ambazo sasa hazifanyiki kutokana na uwepo covid-19.

“Wasaidizi wa kisheria wanaendelea kutumia mbinu mbadala kuwafikia wananchi ikiwemo kuongeza matumizi ya redio hususani redio jamii, matumizi ya mitandao ya jamii,” alisema.

Pia wanatoa huduma kwa mtu mmoja mmoja, elimu sehemu za ibada na njia mbalimbali. Lakini pia wameendelea kutoa elimu ya kisheria na virusi vya corona wakisisitiza kanuni za afya, kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko na kunawa mikono vizuri kwa maji yanayotirika.

Akizungumzia ushiriki wa watoa huduma wa msaada wa kisheria kupambana na ugonjwa wa Covid-19, Mkurugenzi Mkuu wa Morogoro Paralegal Centre (MPLC), Flora Masoy alisema “ MPLC ilituma maombi kwa kamati ya Covid- 19 ya mkoa inayosimamiwa na Katibu Tawala ili wasaidizi wa kisheria wafunzwe corona.

“Walifundishwa kutengeneza vitakasa mikono. Lengo ni kutoa elimu kwa wananchi kujikinga na corona. Mafunzo haya yalifanyika, wanatoa elimu kwa jamii wakishirikiana na halmashauri na watoa huduma wa afya wa wilaya,” alisema.

Ng’wanakilala alisema wasaidizi wa sheria wamekieleza kituo hicho wanavyowalinda wafanyakazi wao kwa kupunguza saa za kazi.

Pia alisema wanapeana zamu ya kwenda ofisini na kufanyia kazi nyumbani na kuvaa na kutumia vifaaa vya kujikinga na maambukizi ofisi zao zikiwa na maji ya kunawa na sabuni na wao kujikinga kwa kuvaa barakoa wanapotoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.

Alisema wanafunzi kukaa nyumbani huchochea kuwepo na vitendo vya ukatili wa kijinsia, ongezeko la mimba pamoja na ndoa za utotoni.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametaka ifanyike tathmini katika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi