loader
Picha

Magufuli- Nimeyamaliza na Kenyatta

Rais Dk John Magufuli amesema mvutano kati ya Kenya na Tanzania unaosababishwa na vipimo vya virusi vya corona ni jambo dogo na ameshazungumza na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuumaliza.

Amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakuu wa mikoa ya Tanga, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha na Mara wakutane na wenzao wa Kenya kulimaliza jambo hilo.

"Wapange ndani ya wiki hii wayamalize haya, haya mambo ni madogo madogo sana... kwa hiyo corona isije ikawa chanzo cha migogoro cha kutokuelewana" amesema Rais Magufuli.

Amewaomba viongozi wa mikoa ya Tanzania inayopakana na Kenya wasitatue matatizo kwa jazba, watangulize Utanzania na Ukenya kwa kuzingatia uchumi wa nchi hizo.

"Na kwa vile tumezungumza vizuri na Mheshimiwa Kenyatta sisi tumeyamaliza, wakae viongozi walitatue hili tatizo na watu wafanye biashara katika pande zote mbili...nataka Wakenya na Watanzania wafanye biashara yao vizuri"amesema Rais wakati akizungumza na wananchi mkoani Singida.

Amewataka madereva watulie kwa kuwa mvutano uliopo utamalizwa na Serikali za Tanzania na Kenya.

"Kwa hiyo niwaombe viongozi katika mipaka hiyo wakae wayajadili haya kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili. Huu ni wakati wa kujenga uchumi. Na corona wala haikuanzia Afrika, imeanzia huko mbali. Na corona imewacoronea wengi kweli hata wale wenye uwezo sasa tusije sisi tukafika ndani ya East Afrika Community tukachonganishwa tukapata kirusi cha kushindwa biashara kwa kisingizio cha corona" amesema.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi