loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mufti Mkuu Zanzibar aelekeza mfumo sherehe za Idd

OFISI ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imesema sherehe za Baraza la Idd hazitafanyika katika mfumo uliozoeleka wa waumini wa dini ya Kiislamu kukusanyika na kufanya sala ya pamoja ya kitaifa.

Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Shehe Khalid Ali Mfaume akizungumza na waandishi wa habari, alisema Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein anatarajiwa kulihutubia Baraza la Idd kupitia vyombo vya habari kuanzia saa nne.

Shehe Mfaume alisema hatua hizo ni ili kuchukua tahadhari ya kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona kupunguza mikusanyiko inayoweza kusababisha maambukizi mapya.

“Tulikuwa tumezoea Baraza la Idd waumini wanakusanyika pamoja na Rais wa Zanzibar kutoa hotuba yenye mnasaba wa sherehe hizo na kupata vinywaji.... mwaka huu kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa corona tumebadilisha mfumo na rais atazungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari,” alieleza Shehe Mfaume.

Aidha, alisema ibada ya sala ya Idd zitafanyika kupitia katika misikiti ya waumini mbalimbali katika maeneo yao na hakutakuwa na sala ya pamoja ya kitaifa.

Alizitaka kamati za misikiti kuhakikisha zinafuata masharti ya kujikinga na corona ikiwemo kufupisha ibada hizo pamoja na hotuba. Waumini wa dini ya Kiislamu nchini na duniani kote wanatarajiwa kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitr, Jumapili au Jumatatu kulingana na mwandamo wa mwezi wakihitimisha mfungo wa mwezi wa Ramadhani ambao ni miongoni mwa nguzo tano za dini ya Kiislamu.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi