loader
Picha

Wanaojifungulia vituo vya afya wafikia 83%

SERIKALI imesema idadi ya akinamama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya, imeendelea kuongezeka hadi kufi kia asilimia 83, ikilinganishwa na asilimia 64 ya mwaka 2015/16.

Hayo yalielezwa bungeni jana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa kujibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Josephine Genzabuke (CCM).

Akiuliza swali lake, Genzabuke alisema: “Asilimia 75 ya vifo vya akina mama vinavyotokea wakati wa ujauzito na kujifungua vinaweza kuepukika. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha akina mama hasa waishio vijijini wanajifungua salama?”.

Katika majibu yake, wizara hiyo ilisema kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeboresha vituo vya afya zaidi ya 352, na vingine kujengwa upya ili vitoe huduma zote za afya ya uzazi kabla na wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua ikiwemo kumtoa mtoto tumboni kwa njia ya operesheni, na kuzijengea uwezo wa kutoa huduma ya damu salama kwa watakaohitaji.

Pia hospitali mpya 67 za halmashauri, zinajengwa ili huduma ziwafikie wananchi wote wa vijijini na mjini kwa usawa na urahisi zaidi. Aidha, katika kuhakikisha kwamba dawa na vifaa tiba vinakuwepo muda wote, serikali imeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Sh bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi Sh bilioni 200 mwaka 2019/20.

Ongezeko hili la kibajeti na usimamizi imara wa rasilimali, limeongeza upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma kutoka asilimia 53 mwaka 2015/16) hadi kufikia asilimia 94 mwaka 2019/2020 Aidha, juhudi hizi zimewezesha wajawazito kuendelea kupata huduma za afya ya uzazi na mtoto, ikiwemo kinga tiba dhidi ya malaria (SP), Fefol ambayo ni kinga tiba dhidi ya upungufu wa damu, vipimo vya shinikizo la damu, kaswende, wingi wa damu, sukari.

“Sanjali na hilo, idadi ya akinamama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 83 mwezi Machi 2020 ikilinganishwa na asilimia 64 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015/16”ilisema.

Wizara hiyo ilisema Novemba 6, 2018, Makamu wa Rais, Samia Suluhu alizindua kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma. Kampeni hiyo ya kitaifa inalenga kuzuia

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi