loader
Picha

Yamekwisha mpakani

Serikali ya Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kuhakikisha madereva wa nchi zote mbili, wanapimwa vipimo vya maambukizi ya ugonjwa wa corona katika nchi husika na kupewa cheti, ambacho watakaa nacho kwa siku 14.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe (pichani) wakati akisoma maazimio ya kutatua mgogoro wa madereva hao maeneo ya mipakani, jana.

Kamwelwe alisema katika kikao hicho cha pamoja kati ya Waziri wa Uchukuzi wa Kenya na Tanzania pamoja na wakuu wa mikoa ya mpakani kutoka Tanzania na Kenya, wamekubaliana kwamba madereva hao baada ya siku 14 watapimwa tena huko huko waliko.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba kuwa endapo siku 14 watapimwa tena nchini Kenya au Tanzania na wakakutwa wana maambukizi, watarudishwa nchini kwao kwa sababu kila nchi ina taratibu zake.

“Tumekubaliana madereva wetu upande wa Tanzania, wapimwe maambukizi ya Covid - 19 kutoka Tanzania na watapewa cheti endapo hawana maambukizi waendelee na safari zao. Na siku 14 zikipita wakiwa nchini Kenya, watapimwa huko huko na wakibainika wameambukizwa watarudishwa nchini”, alisema.

Hali hiyo pia itakuwa kwa upande wa Kenya. Alisema Tanzania haiwezi kuzuia biashara kutoendelea, kwa sababu ya imechukua tahadhari mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo, hivyo hata kama ugonjwa huo upo, lakini lazima shughuli za maendeleo ziendelee.

Waziri wa Uchukuzi kutoka Nchini Kenya, James Macharia alisema kwa upande wa Kenya kipimo cha Covid - 19 kitaanza kufanya kazi mpakani siku ya Jumatatu Alisema madereva wataendelea kupimwa joto ili tahadhari ziweze kuchukuliwa.

Kuhusu maambukizi ya virusi vya corona, watapimwa maeneo husika na kupewa cheti. Alisema masuala mengine ya jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa corona, watayapelekwa kwa wakuu wa nchi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema maelekezo ya jana yamelenga zaidi katika usafirishaji.

Kuhusu masuala ya kijamii, alisema watakuwa wakishirikiana mara kwa mara, kutatua changamoto zitakazojitokeza. Nao baadhi ya madereva wa malori, walisema wanaishukuru serikali kwa kutatua suala hilo la kupima katika hospitali zilizopo nchini Tanzania na kupewa cheti ili waendelee na safari zao.

Walisema awali walikuwa wakipimwa na kuwekewa utepe maalum na walikuwa hawaruhusiwi kushuka sehemu yoyote hadi wafike eneo husika, jambo ambalo ni la ajabu.

NTAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoa ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Namanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi