loader
Picha

CCM yampongeza JPM alivyokabili corona

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais John Magufuli kwa ujasiri wa kutoyumbishwa na wasioitakia mema nchi na kwa kuchukua hatua kuu tatu zilizochochea mafanikio makubwa dhidi ya vita ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid 19).

Hatua hizo tatu ni msimamo wake wa kumuweka Mungu mbele katika vita hii na kusisitiza Watanzania wamuombe sana, pili ni maelekezo yake kwa wananchi kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya na miongozo ya Serikali na tatu ni kuhamasisha Watanzania kuendelea kuchapa kazi bila kufunga mipaka wala kuizuia mikoa iliyoathirika zaidi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikati na Uenezi, Humphrey Polepole, alitoa kauli hiyo ya chama hicho kwa umma kupitia waandishi wa habari jana, katika Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba, Dar es Salaam. Alisema Rais Magufuli ameifanya Tanzania ioneshe njia sahihi ya mapambano dhidi ya virusi vya corona inayoigwa sasa na dunia nzima.

“Chama kinampongeza Rais katika kusimamia nchi bila kuyumbishwa na wasiomtakia yeye na sisi mema. Wale wenye nia ovu, walimbeza yeye na walitubeza sisi kama Taifa, wakatubashiria mabaya na yasio kuwa na neema kwa taifa la Tanzania lakini ukweli ni kwamba Mungu wetu wa mbinguni ameendelea kuwa na sisi na anatuvusha salama.

“Tunatambua huu ugonjwa bado upo lakini tunaendelea kwa kasi kubwa kuushinda na kuishinda vita hii. Rais Magufuli ni mwenye maono, amekuwa mfariji mkuu kwa Watanzania. Kila tulipotetereka na kuhangaika na imani yetu alitutia moyo kuwa tutashinda, tutavuka, tuendelee kuchapa kazi kwa kusimamia maelekezo ya wataalamu wa afya na serikali. Akasema janga hili nalo litapita kama mengine,” alisema Polepole.

Polepole alisema falsafa ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea imejidhihirisha tena tangu ugonjwa huo uingie baada ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutengeneza mavazi ya kinga na kuendeleza vita kwa mbinu za ndani zisizo za kuiga huku akisisitiza kuwa Tanzania si Uchina, Marekani wala Canada iendeshe vita kwa mbinu za kuiga bila kujiongeza.

Alirejea shinikizo la watu wa ndani na nje ya nchi waliotaka baadhi ya mikoa ikiwamo Dar es Salaam ifungwe (lockdown) na kueleza kuwa Rais Magufuli aliona mbali akajua akili za kuambiwa achanganye na zake, akawaza asilimia kubwa ya Watanzania wanapata kipato kwa siku kwa kazi za kujiajiri na kukataa kufunga baadhi ya mikoa na mipaka ya nchi.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliwataja Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT-Wazakendo Kabwe Zitto kuwa miongoni mwa viongozi wa upinzani waliotaka mikoa ifungwe huku wakijua kwa kuwa ni wabunge wao watapata mishahara ya Serikali bila kuwajali mama lishe na wavuvi na kutaka Oktoba watu kama hao wanyimwe kura.

Polepole alisema nchi imeshuhudia madhila makubwa kwa mataifa yaliowafungia watu ndani yakiwamo yalioendelea na hatua hiyo ingefanyika nchini ingeleta matatizo makubwa kuliko ugonjwa wenyewe na kutaka Watanzania kuwapuuza wenye nongwa na nchi na wanaosaka umaarufu kwenye shida.

NTAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoa ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi