loader
Picha

Polepole: Mchakato wa kuandika Ilani ya CCM umekamilika

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mchakato wa kuandika Ilani yake ya mwaka 2020-2025, iliyojaa fursa ambazo hazijawahi kuwepo na mwelekeo wa sera, umekamilika.

Pia, chama hicho kimeunda kundi la mtandao wa Whatsapp, kupokea taarifa za wanachama wake wanaovuruga uchaguzi majimboni. Aidha, chama hicho kimetangaza kiama kwa wanachama hao, wakiwamo watumishi wa serikali wanaojipitisha majimboni na katika Kata, kufanya kampeni kabla ya wakati na kujinadi.

Alisema kuwa chama kinawafahamu watu hao na wasahau kupata dhamana ya uongozi ndani ya chama. CCM pia imetangaza kufungua shughuli zote za chama hicho, baada ya serikali kupitia Rais Dk John Magufuli Jumapili iliyopita, kueleza mafanikio yaliyopatikana katika vita ya kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid 19) unaosababishwa na virusi vya corona.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole (pichani) alisema hayo jana wakati akitoa kauli ya chama hicho kuhusu masuala mbalimbali ikiwamo janga la virusi vya corona katika O fisi Ndogo za CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari. Polepole alisema mchakato wa kuandika Ilani na mwelekeo wa Sera, umekamilika na hivi karibuni baada ya vikao vya chama kukaa, Ilani hiyo itaelezwa kwa umma.

“Ilani ya CCM ni nzuri nzuri mno, ina fursa kubwa hazijapata kuwepo, tutawatangazia baada ya vikao” alisema.

Kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika O ktoba mwaka huu, alisema chama kinasisitiza wanachama wake kutumia muda huu, kufuata katiba na kanuni zake. Kwamba wanaCCM watakaopenda kuomba dhamana ya uongozi, wafahamu uongozi hautafutwi, bali hupewa mtu anayestahili.

“Chama kinatambua wapo wanaofanya vurugu kwenye majimbo ya uchaguzi na kata, tunawafahamu wote, tuna ushahidi wenu wa sauti, video, picha na barua za malalamiko. Nataka kuwatangazia kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi wavurugaji wote na walioanza kampeni kabla ya wakati hawatapewa dhamana ya uongozi kwenye chama,” alisema Polepole. Aliwaonya pia baadhi ya watumishi wa serikali, ambao wamekuwa wakifanya vurumai kwenye majimbo.

Aliwakumbusha kuwa wamepewa dhamana kwenye serikali na Rais, hivyo wafanye kazi zao zikamilike na kama watahitajika kupewa dhamana nyingine, watapewa. Kuhusu shughuli za chama kuanza, Polepole alisema baada ya kufuatilia na kutathimi hali na muelekeo wa ugonjwa wa virusi vya corona, CCM inatangaza kuanza kwa shughuli zake, ila kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya na Serikali.

“Tukipata taarifa zozote tuzijulishe mamlaka ya Chama na serikali, waoga kama chama cha Mbowe (Freeman-Chama cha Demokrasia na Maendeleo), Zitto (Kabwe-ACT-Wazalendo) na Maalim Seif (Sharif) waendelee kujifungia. Sisi tuwatumikie wananchi kuelekea O ktoba, Uchaguzi Mkuu,” alisema.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi