loader
Picha

Wafanyakazi 3,000 Kilombero Sugar walilipwa madai yao yote

SERIKALI imelithibitishia Bunge kuwa malipo yote ya kisheria ya waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, yalilipwa na hakuna madai yoyote yanayodaiwa.

Hayo yameelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa kujibu swali msingi la Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (CHADEMA). Katika swali lake, Haule alisema, “Zaidi ya wafanyakazi 3,000 wa kilichokuwa Kiwanda cha Kilombero walipunguzwa mwaka 2000 wakati wa kubinafsisha kiwanda hicho chini ya mwekezaji wa ILLOVO na mpaka sasa bado hawajalipwa stahiki zao.”

Haule alitaka kujua ni lini serikali itawalipa mafao wafanyakazi hao wa kiwanda hicho, maarufu kama Kilombero Sugar. Wizara hiyo ilifafanua kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, waliachishwa kazi mwaka 2000 na walilipwa stahili zao za kisheria saba.

Stahiki hizo zinajumuisha mshahara wa mwezi mmoja, malipo ya likizo, nauli za watumishi na familia zao, gharama za mizigo, mshahara wa mwezi mmoja kwa kila mwaka kwa kipindi cha miaka 10, malimbikizo ya mishahara ambayo haikulipwa na makato ya michango ya mifuko ya hifadhi ya Jamii (PPF na NSSF). Kiasi kilicholipwa kwa wafanyakazi hao baada ya kuachishwa kazi kilikuwa ni Sh 2,404,984,239.

“Hata hivyo, baada ya malipo hayo wafanyakazi hao hawakuridhika nayo na hivyo kupelekea serikali kufanya uhakiki wa kina wa madai hayo mwaka 2000. Taarifa ya uhakiki ilibaini kuwa kulikuwa na upungufu wa jumla ya shilingi 11,830,019 katika malipo ya awali ambazo serikali ilizilipa,” wizara ilibanisha.

Aidha, baada ya kukamilika malipo ya kisheria, wafanyakazi hao waliendelea kudai malipo ya utumishi wa muda mrefu ya Sh bilioni 1.27 kwa madai ya kuwepo kwa makubaliano ya mkataba wa hiari kati ya Chama cha Wafanyakazi wa kampuni hiyo (OTTU) na menejimenti ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi