loader
Picha

Majaliwa kuwagawia wakulima miche ya michikichi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma kwa ajili ya kugawa miche ya michikichi kwa makundi mbalimbali ya wakulima.

Hatua hiyo ni ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa mkakati wa serikali, kuelekea kujitegemea kwa mafuta ya kula, yatakayozalishwa kupitia zao la michikichi.

Mkuu wa Mkoa Kigoma, Emanuel Maganga aliwaeleza waandishi wa habari mjini Kigoma jana kuwa mpango wa ugawaji wa miche hiyo, utafanyika katika Gereza la Kwitanga katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Kambi ya JKT Bulombora wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Maganga alisema kuwa jitihada kubwa zilizofanywa na Majaliwa, sasa ndiyo zinaanza kutekelezwa rasmi kwa miche iliyozalishwa kupelekwa kwenye mashamba ya wakulima na kupandwa.

Akizungumzia nafasi ya mkoa katika kusimamia utekelezaji wa mpango huo, Maganga alisema kuwa wataalam na watendaji wa mkoa huo, wakishirikiana na taasisi mbalimbali wamejipanga kufanya uhamasishaji kwa wananchi, kutoa maelekezo na kufanya tathmini juu ya mpango huo.

Kwamba tayari wananchi wameonesha ari kubwa ya kushiriki kwenye utekelezaji huo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya alisema kuwa tayari miche milioni 1.8 ipo tayari kwa ajili ya kupanndwa mashambani, ikiwa ni sehemu ya mpango wa uzalishaji na usambazaji kwa wakulima miche milioni tano, Miche hiyo itapandwa kwenye mashamba ya wakulima ili kufikia lengo la Tanzania kulima zao la michikichi kwa wingi kwa ajili ya kujitegemea katika uzalishaji wa mafuta ya mawese na kuondoa hali ya sasa ya kutumia Sh bilioni 445 kuagiza mafuta ya mawese nje ya nchi.

Kusaya alisema kuwa katika mpango wa muda mrefu wa wizara hiyo, wanatarajia kuzalisha miche milioni 15 kwa mwaka na kuisambaza kwenye mashamba ya wakulima na kuwezesha Tanzania kufikia lengo la kuzalisha tani 570,000 kwa mwaka. Uzalishaji huo utatimiza ndoto ya nchi, kuacha kuagiza nje mafuta ya mawese na kufanya manunuzi makubwa kwa fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa hiyo.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi